Na Mwandishi wa Xdeejayz Mtwara
Katika hali ya kusikitisha nay a ukali wa hali ya juu
dereva bodaboda aliyefahamika kwa jina moja la Mbikano anasakwa na jeshi la polisi Mkoani Mtwara kwa
kusababisha mauji ya mtoto mdogo ambae alimgonga wakati akiendesha bodaboda
yake na kumuumiza mguu kisha akambeba na kukimbia nae na baadae kumtupa kwenye
kichaka na fisi wakaja kumla na kubakisha kafuvu kadogo tu.
XDEEJAYZ
INAKUBA ISHU NZIMA:
Habari za
uhakika zilizonaswa na mwandishi wa Xdeejayz aliyeko Masasi na Mtwa zilisema
tukio hilo la kusikitisha limewaliza watu wengi, akiongea na xdeejayz kwenye
mahojiano maalum mjomba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mjomba wa
mrehemu Yusuph Hashim (30) alisema tukio hilo lilitokea tarehe 29, saa 12:30 jioni.
Mjomba huyo
aliendelea kueleza kuwa siku hiyo mtoto huyo aliyeitwa kwa jina la Shabiru Muhidin (4) ambapo wanaishi
katika Kijiji Mkaseka wote na mtoto huyo muda huo alikuwa ametumwa dukani na
mamaake mzazi aliyefahamika kwa jina la Thawabu Hakhim Nakanje.
Hata hivyo
katika ha ilisiyotajia mjomba huyo alisema kuna kundi la vijana waliokuwa
wanatoka kwenye kutizama mpira kwenye kijiji cha Jirani cha Mkururu huku wakiwa wamepakizana kwenye
bodaboda walivyofika maeneo ya Mkaseka ndipo walipomgonga mtoto huyo na
kumjeruhi mguuni na walipoona watu wameanza kujaa ndipo walipomchukua mtoto
huyo ambae alikuwa akilia kwa uchungu na kuondoka nae kusikojulikana.
Mjomba huyo
aliendelea kuileza xdeejayz kuwa kijana huyo aliyekuwa anaendesha bodaboda
aliendelea kutokomea kizani na mtoto huyo hadi alipofika mahali penye msitu
mkubwa alimrusha kichakani huku mtoto huyo alimsihi asimuache msituni hapo
kwani angeliwa na wanyama lakini bila huruma dereva huyo wala hakujali hatimae
alimuacha mtoto huyo.
Habari zaidi
ziliendelea kusema huku nyuma alipogongewa mtoto habari zilianza kusambaa
ambapo mjomba huyo alipopata taarifa hizo aliondoka na majirani zake kuelekea
kwenye zahati ya kijiji hicho kwa kudhani huenda watu hao waliamua kufanya
ubidamu kwa kumpelekea hospitali baada ya kumuumiza ambapo alipofika kwenye
zahati hiyo hakumkuta mtoto huyo.
Baada ya
kumkosa kwenye zahati hiyo walienda kwenye kituo kikubwa cha Afya cha Nagaga
lakini hapo napo hawamkuta ndipo walishauriana kwenda kuripoti kwa mkuu wa
polisi jamii na mara baada ya kukutana na kamanda wa polisi jamii aliyefahamika
kwa jina la Hamis na baada ya kuwasikiliza aliitisha kikao cha dharula na
wakaanza kumtafuta mtoto huyo hapo ilishakuwa siku iliyofuata ambapo baada ya
msako kfanyika walienda hadi kwenye sehemu moja yenye kilima msitu.
Baada ya
kufika kwenye mlima huo waliona mburuzo ulioambatana na damu na walipoenda mbele
zaidi waliona damu nyingi zikiwa na vimetapakaa na vipande vya utumbo na fuvu
kipande kidogo tu hali waliyogundua kuwa mtoto huyo alishapoteza uhai wake kwa
kuliwa na fisi ambao eneo hilo wako wengi kama mbuzi.
Kufuatia
kushuhudia hayo kamanda wa ulinzi shirikishi alipiga simu kituo cha polisi
Masasi ambapo polisi walifika haraka na kupiga picha eneo la tuki huku
wakiondoka na mabaki ya fuvu hilo kwa ajiliya uchunguzi zaidi.
Hata hivyo
hadi sasa mliki wa bodaboda hiyo anashikiriwa na jeshi la polisi huku mtuhumiwa
namba moja akitafutwa kwa udi na uvumba ili kufikishwa mbele ya mkono wa dola.
Xdeejayz ilifanya jitifahada za kumtafuta kamanda wa polisi
Mkoa wa Mtwara ili kuzungumzia ambapo
baada ya kupigiwa simu ilipokelewa na mlinzi wake huku akisema kuwa Kamanda
yuko bize na vikao hivyo atafutwe jioni ya leo.
No comments:
Post a Comment