Marehemu Robert Mwandisi enzi za uhaki wake na picha hizi alipiga siku moja kabla ya kifo chake.
Haya ni mabaki ya sehemu ya gari hii ya thamani kubwa aina ya Lange Lover sport kama inayoonekana ambayo marehemu alikuwa kitumia kwenye shughuri zake za kazi.
Na Mwandishi
Wetu
Mmiliki wa
baa na Club za Matema Annex Park zenye umaarufu mkubwa Jijini Dar hasa
Kinondoni aliyehamika kwa jina la Robert Mwandisi amepoteza maisha baada ya
kupata ajali mbaya maeneo ya Daraja Mbezi Chini kwenye daraja la Kawe.
Xdeejayz
ambayo imefika kituo cha polisi Oysterbay na kushuhudia gari hiyo aina ya Range Lover Sport yenye namba za usajili T660
CEP ikiwa imeharibika vibaya kwa hali ya muonekano wa gari hiyo isingekuwa
rahisi kutoka mtu akiwa salama.
Habari zaidi
kuhusu chanzo cha ajali hiyo iliyotokea saa kumi za usiku ambapo wakati
marehemu akifikwa na balaa hilo alikuwa akitokea kwenye mizinguko ya biashara
zake na alikuwa kirejea nyumbani kwake mbezi beach na alipofika maeneo hayo
gari yake ambayo ilielezwa ilikuwa kwenye kasi kubwa iliacha njia na kupinduka
zaidi ya mara sita hali iliyosababisha ijikunje kama chapatti.
Hata hivyo
meneja Promotioni wa Club ya Jacaranda iliyopo maeneo ya Mango Garden
aliyefahamika kwa jina la Maneno ametoa ratiba ya msiba wa marehemu bosi wake
kama ifuatavyo
Siku ya Jumanne
asubuhi Saa 2 kutakuwa na ibada ya misa ya kumuombea marehemu nyumbani kwake
Mbezi,Baada ya misa litafuata tendo la kuuaga mwili wa marehumu baada ya
shughur za kuaga kumalizika safari ya kuelekea Kyela Mkoani Mbeya itaanza na
huko ndiko utakapoenda kupunzishwa mwili wake katika makao yake ya milele.
Marehemu
Robart ameacha mjane mmoja na watoto wawili
Kwa niaba ya
kampuni Entertainment Masters Ltd na
bodi ya wakurugenzi pamoja na wafanya kazi wote wa Club Maisha Mbeya, Dar,
Ntwara, Mwanza na Dodoma wanaungana na familia ya marehemu kwenye kipindi hiki
kigumu cha kuondokewa na ndugu yetu kipenzi kimsingi pengo lake halitozibika
daima kwetu kwani tulishirikia na marehemu mambo mbalimbali ya kibiashara nk
lakini kwa sasa hatuna budi kumshukuru mungu kwa kazi yake ambayo daima haina
makosa.
MUNGU AMETOA
NA SASA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE AMEN.
No comments:
Post a Comment