Wakati kukiwa na madai ya Jeshi la Syria limetumia silaha zenye kemikali kuwashambulia waasi na kusababisha madhara makubwa huku Ris Obama akitoa tamko la wzi kuwa anafikiria kusaini ili kuruhusu Syria kuchapwa kumbe kuna taarifa kuwa tayari makomdoo wa kimarekani wameshatua nchini humo siku nyingi tu.
Habari za uhakika toka kwenye moja ya mitandao ya nchini Marekani zilionesha shehena ya mabomu huku wanajeshi wa marekani Makomandoo wakiwa kwenye mazoezi makali nchini Syria huku wakisubiri sekunde ifike waanze mashabulizi hatari.
Aidha hata kauri aliyoitoa Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel kuwa Marekani inaweza kuishamburia Syria bila uchunguzi wa timu ya umoja wa mataifa na sasa imejidhilisha kwani wadadisi wa mambo wanasema hata hizo kauri za rais Obama kusubiri kusaini ni zuga tu kwani tayari majeshi ya Marekani yapo nchini humo.
Wakati huo huo Serikali ya Urusi imeapa kuiunga mkono Syria hadi hatu ya mwisho. Akiongea na magazeti ya nchi Urusi yalimnukuu waziri wa habari wa Urusi Omran Zoabi akiionya marekani kuwa itashindwa vibaya katika vita hiyo kama itajaribu kuishambulia Syria.
Hata hivyo inadaiwa kuwa Marekani itakachokifanya awali nchini Syria ni kuvamia miundo mbinu ya nchi hiyo kwa kuharibu pamoja na kushambulia maghala yote ya silaha kubwa ili kulimaliza nguvu jeshi la Serikali.
No comments:
Post a Comment