Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kupitia
kitengo cha maudhui imevifungia matangazo kwa muda wa miezi sita vituo vya radio
viwili nchini kwa kukiuka maadili ya
utangazaji.
Vituo hivyo ni pamoja na Kwa
Neema FM ya Mwanza iliyofungiwa kwa kuendesha mjadala uliokuwa ukihusiana na
watu wa dini gani wenye haki ya kuchinja wanyama kati ya waislam na wakristu
hali iliyosababisha mgongano wa waumini wa dini
hizo.
Kingine ni Imani Radio FM ya mjini Morogoro ambayo
imefungiwa kwa kosa la kupinga zoezi la sensa mwaka jana na kuwashawishi waumini
wa dini ya kiislam wasijiandikishe.
Nayo Clouds FM imepigwa
faini kwa kuendesha mjadala kuhusiana na ushoga pamoja na kuwa na kipengele
kwenye kipindi cha Power Breakfast kiitwacho ‘Jicho la Ng’ombe’ ambacho
wametakiwa wakifute kutokana na kuendeshwa kinyume na maadili
|
No comments:
Post a Comment