Mmoja wa watangazaji wa kituo hicho cha radio cha E-FM 93.7 JohnBosco katikati akitimiza majukumu yake kwenye zoezi la kuwajazia mafuta full tank madereva wa Bajaji na bodaboda maeneo ya mbezi beach jana ilikuwa balaa.
Deveja wa bodaboda akifurahi kuzajiwa mafuta na 93.7 E-FM
Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu ywa 93.7 E-FM, Sos B akiangalia kwa umakini zoezi hilo jinsi linavyoendeshwa na vijana wake.
Na Livingstone Mkoi
Siku ya jana ilikuwa ya neema kwa waendesha bodaboda wa maeneo ya Mbezi Beach Jijini Dar kufuatia kampeni kabambe ya radio mpya ya 93.7 E-FM kuwapatia zawadi madereva hao kwa kuwajazia mafuta full tank kwenye vyombo vyao.
Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo ambae pia ni kiongozi wa kituo hicho Sos B aliiambia Xdeejayz kuwa" Tumeanza program hii kwa mashabiki wetu ambapo hii itakuwa oparesheni ya Jiji zima la Dar na tumeanzia Mbezi lakini tutazunguka mji mzima na ole wako ukutwe na stika za radio hiyo inayopatikana na 93.7 basi hapo hapo wahudumu wetu watakujazia mafuta full tank" Alisema
Aidha zoezi hili lilifana sana kufuatia kuripotiwa live radion ambapo madeva zaidi ya mia tatu walifika kwa ajili ya kujaziwa mafuta, na wiki ijayo zamu ya sehemu nyingine ambayo itatangazwa kupitia radio hiyo mpya ya burudani.
No comments:
Post a Comment