TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Sunday, January 6, 2013

MAMA MZAZI WA SHARO MILIONEA ATOA KAULI NZITO KWA WASANII KWENYE AROBANI YA MWANAE!

 Marehemu Sharo Milionea ambae jana tarehe 5 Januari ilikuwa siku ya arobaini yake. Na shughuri mbalimba za kisomo zilifanyika nyumbani kwa Tanga.
 Mama Mzazi wa Shalo Milionea.
                                      Mama Mzazi wa Shalo Milionea.
Na Livingstone Mkoi
Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa komedy na muziki wa kizazi kipya Sharo Milionea jana alitoa kauli nzito kwa wasaniii wote walifika kwenye shughuri ya arobaini ya mwanae huyo ambae alikuwa kipenzi chaa watu nchini iliyofanyika jana tarehe tano Mkoani Tanga.
Shughuri hiyo iliyohudhuliwa na watu kiasi chake kutokana na watu wengi hasa wasanii wa filamu kushindwa kwenda kutokana na mambo kuingiliana hasa baada ya msiba wa Sajuki.
Hata hivyo licha ya mambo hayo kuingiliana lakini Rais wa shirikisho la filamu Tanzania "TAFF" Saimon Mwakifwamba aliweza kuongoza msafara wa wasanii wa Komedy hadi Tanga na kuweza kushirikai shughuri hiyo baraba.
Msafara wa wasanii hao ulifika saa saba za usiku ambapo ulikuta visomo vikiendelea ambapo hadi kufikia asubuhi kila kitu kilikuwa tayari pamoja na chakula ambacho kwa kiasi kikubwa kilichangiwa na wasanii wa komedi kupita chama chao walichokianzisha hivi karibuni Tanzania Comedian Asosiation"TCA".
Aidha hadi kufikia saa sita mchana siku siku hiyo ya Jumamosi shughuri zote zilikuwaa zinaelekea ukingoni.Lakini hata hivyo kabla watu hawajatawanyika wanakomedi hao ambao walikuwa na mchango wao ambao walikuwa wameuchanga kabla ambao ni kiasi cha shilingi Milioni Moja"1000,000/= waliendaa kumkabidhi mama mzazi kwa ajili ya kufungua biashara ndogo ndogo.
Hata hivyo baada ya tukio hilo la kumpatia mchango huo.Mama mzazi huyo kwa busara alianza kuwaeleza kutoa kauli za kuwahusia wasanii hao kama hivi" Wanangu kwanza nashukuru kwa msaada wenu kwa kweli mmenionesha ushirikiano wa hali ya juu tangu mwenzenu alipotutoka hivyo hivyo ushirikiano huo usiishie hapo naomba pendaneni chuki huwa ni laana kwa mwenyezi Mung" Hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya mama huyo
Aidha Mama huyo anaendelea kuwashukuru watanzania kwa ujumla kwa kumufariji tangu alipoondokewa na mwanae hawazi kuwataja mmoj mmoja lakini anawaombea kwa mungu wote.

No comments:

Post a Comment