TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, October 31, 2012

BOB JUNIOR APONDA NGOMA MPYA YA DIAMOND.




Rais wa Mashorobaro.


Nyota wa ngoma ya mawazo ambaye pia ni bosi wa lebo ya Sharobaro Record, ya jijini Dar, Bob Junior amesema sasa yuko tayari kusimama kwenye ngoma moja na mkali kutoka Wasafi Entertainments, Diamond Platinumz.

Akizungumza na xdeejayz, mapema leo Bob Junior amesema licha ya kuwa aliwasili jana jioni kutoka Oman alikokuwa kwa mapumziko na amepata bahati ya kuisikiliza ngoma mpya ya Diamond na kuona kuwa ni ya kawaida kwani haina kitu kipya ilichofanyiwa.

Diamond.

"Unajua kwa sasa mimi nimewapisha vijana wangu kwanza watoe ngoma zao na baada ya wiki mbili nitatoa ya kwangu, ninachoweza kusema ni kuwa sasa niko tayari kusimama kwenye wimbo mmoja na dogo huyo kwani naamini mimi ni mkali zaidi yake na Watanzania wanajua hilo" alisema Bob.

Akiendelea zaidi Bob aliyeitikisa Bongo kwa ngoma kali ya Oyoyo alifunguka kuwa, sasa ana mipango ya kufanya vitu tofauti vitavyosukuma mbele muziki wa kizazi kipya na zaidi akilenga katika kujiongezea mapato tofauti na kutegemea MKWANJA WA shoo au promo za matangazo.

No comments:

Post a Comment