TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, August 29, 2013

MWENDO KASI WAUA 13 PAPO HAPO,11 WAKO MAHUTUTI!


HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA WATU 13, WAMEFARIKI DUNIA NA 11 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA KIJIJI CHA NGONGWA MKOANI SHINYANGA KWENYE AJALI ILIYOHUSISHA GARI AINA YA HICE LENYE NAMBA ZA USAJIRI T 756 CHX NA GARI LILILOKUWA LIMEHARIBIKA LENYE NAMBA ZA USAJILI T 696 AMS.

AKIZUNGUMZA KWA NJIA YA SIMU KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA, KIHEMA KIHEMA, ALISEMA KUWA MIONGONI MWA WATU WALIOFARIKI DUNIA NI PAMOJA NA DEREVA WA HICE, ILIYOKUWA NA ABIRIA HAO IKITOKEA KAHAMA KUELEKEA USHIROMBO AMBAYE ALIFARIKI PAPO HAPO, HUKU MAJERUHI WAKIPELEKWA KUPATIWA HUDUMA YA KWANA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.


KIJANA ALIYETENGWA NA FAMILIA KISA KUOA ALBINO AONESHA MSIMAMO WA HALI YA JUU NA KUSEMA HATOMUACHA MKEWE HADI MWISHO WA UHAI WAKE!



KIJANA aitwaye Priscus Mushi, mkazi wa Mbezi jijini Dar ambaye ni muumini wa Kanisa la Efatha linaloongozwa na Mchungaji Josephat Mwingira ameanika masikitiko yake baada ya kutengwa na baadhi ya ndugu kufuatia kuoa mlemavu wa ngozi ‘albino’ aitwaye Tumaini Murungu.

Akizungumza katika Ukumbi wa Maji uliopo maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo sherehe za ndoa zilifanyika, Mushi alisema alipotangaza nia ya kumuoa Tumaini baadhi ya ndugu zake walimtenga lakini hakukata tamaa kwani aliendelea na taratibu za ndoa.

“Nilimpenda sana Tumaini na niliamini ndiye mwanamke wa maisha yangu lakini nilipowaambia ndugu zangu kuwa nataka kumuoa, baadhi walinitenga kwa uamuzi wangu huo wa kumuoa Tumaini ambaye ni mlemavu wa ngozi eti nitakuwa nimeleta balaa nyumbani.

“Nilimuomba Mungu anisaidie na nikaongea na waumini wenzangu ambao walikubali kunifanyia sherehe.

Nawashukuru sana wakwe zangu ambao walinipokea na kunipa ushirikiano katika kulitimiza tukio hili. Pia nimshukuru mama yangu kwani uwepo wake umenipa faraja kubwa,” alisema Mushi.

Wakizungumzia kitendo cha Mushi kutengwa na baadhi ya ndugu zake, baadhi ya waumini walilaani wakieleza kuwa, si jambo zuri hata kidogo.

“Inaumiza sana, unajua binadamu wote ni sawa, kwani msichana albino hastahili kuolewa? Tuache ubaguzi usiyo na maana ambao unamchukiza hata Mungu.


"Eti kuoa albino ni mkosi kwenye familia, nani kasema? Imani hizi potofu zikemewa kwa nguvu zote,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Eliza.
Hata hivyo kijana huyu amesema kuwa kamwe sitomuacha mke wangu.

UCHEZAJI NUSU UCHI WA SHILOLE WAPONDWA NA WADAU, WASEMA VITENDO HIVYO VINAONGEZA HAMASA YA NGONO NA KUWA KIKAZWA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI!






hatari

GK WA EAST COAST AIBUKA TOKA MAFICHONI, AMEKUJA KUWASHIKA KIVINGINE!




Baada ya kupotea kwenye muziki kwa muda mrefu sana Crazy Gk amerudi kwa kishindo na kuzindua wimbo wake mpya huku akisindikizwa na timu ya East Coast Team.
Sababu kubwa iliyopelekea King Crazy Gk kupotea kwenye game kwa muda mrefu ni kwamba msanii huyu alikuwa kwenye masomo akitafuta degree.

UNYAMA JUU YA UNYAMA MTOTO WA MIAKA 6 ANYOFOLEWA MACHO KWA KISU CHA MOTO, MAMA MZAZA APOTEZA FAHAMU BAADA YA KUMUONA MWANAE AKIWA HANA MACHO WAKATI DAKIKA TANO ZILIZOPITA ALITOKA NYUMBANI AKIWA MZIMA!



Mtoto aliyeng'olewa macho nchini China

Polisi nchini Uchina imetangaza kuwa itatoa zawadi kwa yeyote atakayetoa habari zitakazowasaidia kumkamata mama mmoja ambaye anashukiwa kumng'oa macho mvulana mwenye umri wa miaka sita.
Shambulio hilo linasemekana kutokea tarehe ishirini na nne mwezi huu katika eneo na Fenxi, iliyoko katika mkoa wa Shanxi.
Mvulana huyo anasemekana alikwenda kucheza na watoto wengine lakini wazazi wake walimpata baadaye huku macho yake yote yakiwa yamengolewa huku akivuja damu.

Mvulana huyo kwa sasa anaendelea kupata matibabu hospitalini.

Idara ya polisi nchini humo imetoa zawadi ya zaidi ya dola elfu kumi na sita kwa yeyote atakayetoa habari, kuhusu aliyehusika na shambulio hilo.

Wazazi wa mtoto huyo wanasemekana kuwa wakulima.

Mamake amesema mtoto huyo aliwaambia kuwa wakati alipokuwa akitembea alishambuliwa na mama mmoja ambaye hakumfahamu.

Polisi walipata macho ya mvulana huyo karibu na eneo la tuko.

Uchunguz wa awali umebainisha kuwa sehemu ya mboni au Cornea kwa Kiingereza ilikuwa imengolewa, na hivyo kuashiria ulanguzi wa viungo vya kinadamu.

Hata hivyo polisi wanasema hawajatambua chanzo cha shambulio hilo

Wednesday, August 28, 2013

TAZAMA PICHA 20 ZA YALIYOJIRI KWENYE SHOW YA STR8 MUZIK FREESTYLE MWANZA:

 



WASHINDI WATAKUJA DAR KWA AJILI YA FAINAL

ANT EZEKIA ADAIWA KUFUMANIWA NA MUME WA MTU, ACHANWA VIBAYA NA CHUPA MKONONI!


Aunty Ezekiel.
Ant Ezekiel.mwigizaji wa filamu Swahilihood.
MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Swahilihood Ant Ezekiel imeripotiwa kupata majeraha katika mkono wake wa
kushoto baada ya kuchimbwa na chupa yenye ncha kali, sakata hilo la hatari lilitokea katika Club ya Billicanas wakati wa show iliyokifanyika hapo chini ya Madam Wema Sepetu chanzo chetu kimetuhabarisha.

Aunty Ezekiel
Mkono aliojeruhiwa Ant
Aunty Ezekiel
Ant kama anavyoonekana akiwa kitandani amelazwa..
 Na Mwandishi Wetu
Siri imefichuka na picha kuvuja zikimunesha muigizaji Ant Ezekiel akiwa na jeraha kubwa kwenye mkono wake wa kushoto baada ya kujeruhiwa vibaya na chumba kufuatia kudaiwa kufumaniwa na mume wa mtu huko Club Billcanas.
Habari za toka kwa vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa Ant siku ya tukio Ant alikuwa mmoja wa wageni waalikwa lakini kumbe kwenye mualiko huo alitumia nafasi ya kutoka na mr wa mtu.
Hata hivyo xdeejyz baada ya kupata taarifa hizo ilimtafuta Ant ambae mahala alipolazwa ni siri kubwa lakini kwa bahati mbaya simu yake iliita bila kupokelewa.