Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea tena leo February 6 kwa michezo kadhaa kupigwa, miongoni mwa michezo iliyochezwa leo February 6 ni mchezo kati ya Mouscron FC dhidi ya klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, mchezo huu ulikuwa na mvuto kwa Tanzania zaidi kwani ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta kucheza toka amejiunga na klabu hiyo.
Mbwana Samatta ambaye ndio nahodha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu yake mpya ya KRC Genk akitokea benchi, Samatta aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis ambaye alitoa pasi ya goli la ushindi kwa KRC Genk dakika ya 63 na Thomas Buffel kupachika mpira nyavuni.
Mchezo ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji wao Mouscron, lakini hadi mpira unamalizika Mouscron walikuwa wanaoongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 53 na KRC Genk asilimia 47, ushindi huo umeifanya KRC Genk kutimiza jumla ya point 38 na kusogea hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi. KRC Genk wanarudi tena dimbani February 13 kucheza dhidi ya Waasland-Beveren katka dimba lao la Cristal Arena.
No comments:
Post a Comment