Huyu ni mmojwa aliyekuwa baunsa maaarufu aliyefahamika kwa jina la CHURA kabla ya kufikwa na umauti akiwa Hospital ya Mwananyamala baada ya kukatwa katwa mapanga kichwani eneo la tukio.
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Wakazi zaidi ya elfu 5000 wa kata ya Wazo mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa juzi walifanya kumbukumbu ya kuwakumbuka marehemu wote waliorafiki kwenye migogoro ya ardhi kwenye mtaa huo huku wananchi hao wakimuhusisha Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kuwa kama angekuwa tayari mkuu wa Wilaya basi mauaji hayo yasingetokea leo hii.
Wakiongea na mtandao huu wa habari za uchunguzi wananchi hao walisema " Kiukweli tunawakumbuka ndugu zetu waliopoteza maisha wakiwemo wale mabaunsa waliopigwa mishare ya kichwa na mapanga kisa mgogoro huu wa ardhi ambao kwa sasa Mheshimiwa Makonda anakwenda kuumaliza na tunaamini kama Mheshimiwa Makonda angekuwepo hakika hakuna tone la damu ambalo lingemwagika" Walisema
Hata hivyo wananchi hao wameendelea kumuomba Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kumuongezea majukumu DC Makonda kwa kumpa ukuu wa Mkoa kwani kwa sasa ndiye DC pekee anaefanya kazi usiku na mchana huku mafanikio yake yakionekana hali inayopelekea hata Wilaya nyingine za Jiji la Dar wakihitaji msaada wake.
Hata hivyo licha ya zoezi la uhakiki kubakisha wiki mbili kumalizika, lakini kwa sasa limesimama kidogo kufutia kuwepo kwa mtafaruku wa kati ya mtu aliyedai kuwa hilo shamba lake ambae ilifahamika kama alishaliuza kwa muhindi huku RC na DC Lugimbana wakidaiwa kuwa mashahidi wa mauziano hayo, hivyo kwa sasa eneo hilo lipo chini ya muhindi lakini cha kushangaza muhindi amegoma kujitokeza badara yake amekuja mtu aliyeuza tayari eneo hilo huku kamati za ardhi kata hiyo zikifahamu fika kama huyo mtu eneo hilo halimuhusu tena.
Aidha wakazi hao ambao wengi wao ni wakina mama wanasema wanampango wa kufanya sherehe kubwa ya kumpongeza DC Makonda kwa kazi nzuri ya kutenda haki aliyoifanya bila kuogopa nguvu ya mafisadi lakini pamoja na kigogo mwenye mamlaka kuliko yeye ambae anadaiwa kwenye mgogoro huo anamkono wake.
No comments:
Post a Comment