
Jackie Chan amesema kupitia tukio hilo amejifunza kuwa baba bora kitu ambacho hakukijua siku za nyuma.
Mtoto wa staa huyo, Jaycee Chan alikamatwa kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi zaidi ya gramu 100 ndani ya nyumba yake, na baadaye kushitakiwa kwa kuuza dawa hizo.
Jackie Chan ambaye amekuwa balozi wa kupinga dawa za kulevya tangu mwaka 2009, amesononeshwa na pia ameomba radhi kwa kosa alilotenda mwanae ambapo hii imekuwa mara yake ya kwanza kujibu swali linalohusiana na kesi ya mtoto wake, akisema kupitia hilo amejifunza kuwa baba bora.
No comments:
Post a Comment