Shekh Sharif Khamis ambae kwa sasa amrejea Tanzania akitokea nchini Kanada na Kongo alikokuwepo kwa ajari ya kufanya dua za kuwakomboa watu kwenye matatizo yao.
Mchungaji Kiongozi Amos Mbena wa Kanisa la Pentecostal Holness Mision Bonde la Ukombozi lililopo Kimara Suka mtaa wa Gorani |
Dr Kessy |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda |
Watumishi wa Mungu wa imani zote wamejitokeza na kusema maombi maalum kwa ajiri wa viongozi wa taifa hili ambao dhaihiri wameonekana kupambana na na ufisadi uliokuwa tishio kwenye Serikali iliyopita kiasi cha kuwafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao.
Maskanibongotz kama kawaida yake ilifanya mahojiano maalum na watumishi hao kwa nyakati tofauti ambapo Dr Kessy ambae ni mkurugenzi wa Fiesal
Naturopathic Clinic iliyopo Mburahiti Shule ya Msingi Mianzini alianza kusema " Shekh hakika sisi tunaendelea na dua za kila siku kuwaombe viongozi wetu ili mungu awalinde na kuwapa ujasiri zaidi wa kupambana na hayaoa mambo ya kifisadi"Alisema
Aidha Dokta Kessy aliongeza kusema kuwa Mh Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambae kiukweli amefanyakazi nzuri na ya hatari kutangaza vita na mafisadi wa ardhi kiasi kwamba hadi sasa hali ya amani imeanza kurejea kwa wakazi wa Nakasangwe na Nakalekwa .
Aidha anae Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Holness Mision Bonde la Ukombozi lililopo Kimara Suka mtaa wa Gorani Amos Mbena alisema" Tunapaswa kuungana watu wote wenye nia ya dhati na taifa hili kama tulivyofanya kwenye uchaguzi hivyo tuendelee kuwaombea viongozi wetu wa taifa hili.
Nae kijana Shekh Sharif Khamis ambae amekuwa akiizunguka Dunia kwa ajiri ya kufanya dua ili watu wapate ukombozi ambae kwa sasa amrejea nchini alisema " Taifa hili bado linahitaji dua ya kutosha kuwaombea viongozi wetu, Mh Paul Makonda amejitoa muhanga kupambana na ufisadi wa ardhi kule Nakasangwe na mahara pengine ni jambo ambalo wengi liliwashinda" Alisema kijana huyo na kuwaomba watanzania wote kuendelea kuwaombea viongozi wetu
Credit: maskanibongotz
No comments:
Post a Comment