TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, October 27, 2015

UTAJIRI WA DK FADHILI WAMFUNIKA VIBAYA DIAMOND, ANAMILIKI NYUMBA ZENYE THAMANI TA TSH BILI 3.5..!

   Billgate wa Tanzania Dokta Fadhil juu chini ni moja ya Jumba lake la kifahari ambalo limezusha minong'ono huku akidaiwa kumiki nyumba zaidi ya 10 kama hizo hapa mjini na Jijini Arusha.
Na Anna Mdemu
Kijana wa kitanzania aliyefahamika kwa jina la Dokta Fadhili “ Billget” wa Tanzania utajiri umekuwa tishio kiasi cha kuwafanya watanzania kupigwa butwaa na kushindwa kuamini kama ni yeye kijana mdogo anaweza kumiliki mali hizo.
Wakiongea na gazeti hili wakazi mbali mbali wa jiji la Dar es Salaam walisema “ Jamani huu huyu kijana vipi mbona utajiri wake ni wa kutisha kiasi hicho nyumba anazo Tanzania nzima na ukiangalia kila nyumba hapo haipungui zaidi ya milioni mia tatu na hamsini” Walisema watu wa karibu na Dokta huyo
Aidha  wananchi hao waliendelea kusema kuwa  ubilionea wa kijana huyo hakika hauingii hata robo ya ule wa mwanamuziki Diamond ambapo walifika mbali na kusema inawezekana hata akawa mfanyakazi wake wa ndani kwa fedha alizokuwa nazo.
Kijana huyo ambae ni dokta bingwa wa magonjwa yote amekuwa kivutia kwenye vyombo mbalimbali vya habari hasa kwenye mada zake za kuhufu afya na tayari hadi sasa kasha fanya mahojiano na vituo zaidi ya 50 vya tv na radio na wananchi kunufaika na ushauri wake wa kitabibu.
Gazeti hili lilimtafuta Dokta Fadhili kupitia simu yake ya kiganjani na alipatikana na kueleza  haya “ Mimi nashangaa jinsi watu wanavyopigwa na butwaa kwa mali zangu sielewei dhambi iko wapi mimi kuwa na vitu hivyo ambavyo navimiliki kihalali’ alijibu Dokta Fadhili ambae watu wengi wanahuisha utajiri wake na Freemansonry
Credit: maskanibongotz

No comments:

Post a Comment