TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, October 27, 2015

KIUMBE ANAEDAIWA KUWA NI JINI AZUSHA BALAA KANISANI, WAUMINI WATAFUTA MLANGO WA KUTOKEA..!



 Hapa mara baada ya kuuliwa na wachungaji hao


 Hapa kiumbe huyo akiwa juu ya mti aina  mkorosho
  Wachungaji Inocent Gelvas kushoto, katikati na Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Amos Mbena   na kiongozi wa kanisa hilo Musa Hassan Musa wakimshangaa kiumbe huyo wa ajabu.



Na Anna Mdemu
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua waumini wa Kanisa la Pentecostal Holness Mision Bonde la Ukombozi  lilipo Kimara Suka mtaa wa Gorani Jumapili ya tarehe 18 mwezi huu walitafuta pa kutokea ili kuokoa maisha yako baada ya kiumbe wa ajabu anaedhaniwa kuwa ni jini kuibuka wakati ibada inaendelea.
Mwandishi wa gazeti hili ambae alikuwa mmoja wa waumini waliohudhuria ibada hiyo alishuhudia timbwili hilo la aina yake  ambapo ibada kuu ya Kanisa hilo la wokovu huwa inaanza saa nne asubuhi na kumalizika saa saba mchana na siku hiyo ibada hiyo ilishindwa kumalizka kwa amani kutokana na ghazia hiyo.
Habari zaidi zilieleza kuwa Kanisa hilo  limekuwa kwenye vita kubwa na wachawi kutoakana na mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo aliyefahamika kwa jina la Amos Mbena kuwaumbua vibaya kiasi cha kutishiwa kuuawa na mtandao huo wa wachawi.
Hata hivyo siku ya tukio ilikuwa saa sita na nusu muda mchache kabla ya ibada kumalizika ambapo kanusa hilo lililopo bondeni kidogo huku pembeni yake kukiwa na mti wa mkorosho ambapo chini ya mti huo kulikuwa na watoto wamelala wakisubiri wazazi wao wamalize ibada kasha warejee makwao.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati maombi yakiendelea ya kuwaombea watu wenye shida mbalimbali mchungaji kiongozi wa kanisa hilo kwa mbali kupitia macho ya roho mtakatifu alioneshwa kiumbe huyo wa ajabu mwenye macho kama ya binadamu, huku akiwa na mkono mmoja na mguu mmoja  akiwa juu ya mkorosho huo na haikufahamika kama alikuwa anavizia kuwanyonya dawa watoto ama laa.
Hata hivyo mchungaji huyo aliamua kusitisha ibada kwa muda ili kupambana na kiumbe huyo ambapo baada ya mtumishi huyo wa bwana kumnyooshea mkono  kiumbe huyo alianza kuruka ruka juu ya mtu pamoja na kutoa sauti ya ajabu hali iliyowafanya baadhi ya waumini kuanza kutimua mbio kwa kuhofia usalama wao na baadae sasa kila mtu alimuona live kiumbe huyo wa kutisha.
Baada ya kuonekana kiumbe huyo hatimae ibada iliishia pale pale ambapo jopo la watumishi wa mungu waka kanisa hilo  Inocent Gelvas, , Mchungaji  Musa Hassan Musa wakiongozwa na mchungaji Kiongozi Amos  pamoja na waumini walianza kufanya maombi ya  nguvu ili kurudisha amani kanisani hapo.
Na katika hali ya kushangaza  ghafra kiumbe huyo alipoteza huku wakimsaka bila mafanikio, lakini baada ya nusu saa ghafra kiumbe huyo alidondoka toka kwenye mti huo  huku akiwa hana nguvu ndipo wachungaji hao walipomuua kwa mawe kwa kuponda kichwani kasha kumteketeza kwa moto hadi kuwa majivu.
Baada ya tukio hilo mchungaji kiongozi wa kanisa hili Amos aliongea na mwandishi na kusema haya” Ndugu hii ni vita kubwa na bila nguvu za mungu tusingeweza kuendelea kuwepo mahara hapa huyu sijui nai kiumbe wa aina gani kwani binafsi sijawahi kumuona mahara popote  na sijajua kama ni jini au nini kwa vile binafsi simjui jini sasa huenda  akawa ni mwenyewe” Alisema mchungaji huyo.
Credit: maskanibongotz

No comments:

Post a Comment