Hata
hivyo katika mchezo huo ambao ulianza kwa kila timu kushambulia lango
la mpinzani wake lakini Azam walionekana kucheza faulo nyingi kwa
wachezaji wa Yanga kiasi cha kuwaboa mashabiki kwa kushindwa kutulia na
kucheza mpira mzuri.
Aidha
refa wa mchezo huo alijitahidi kuchezesha fea kwani awali alijaribu
kutumia kuonya kwa mdomo kwa wachezaji wa Azam ambao tayari walikuwa
wamepaniki, hata hivyo isingekuwa kucheza faulo za "Kijinga" na
zisizokuwa za msingi Azam walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda hasa
kwenye kipindi cha dakika ya 84 na 89 kwani Wachezaji wa Yanga
walipoteana kwenye dakika hizo mara baada ya mchezaji wa Azam Kipre Tchetche kurusha goli baada ya Yanga kuongoza kwa dakika zote.
No comments:
Post a Comment