Rais JAKAYA KIKWETE na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimpa pole Mama Sepete baada ya kufiwa na mumewe.
Rais JAKAYA KIKWETE akiwa na wageni wake kwenye moja ya Hafra alizokuwa anaziandaa Ikulu kwa ajiri ya kula pamoja na watoto wasiojiweza
Rais JAKAYA KIKWETE na Mkewe hawakuacha kufika kwenye msiba wa kila kiongozi bila kujari dini yake.
Rais JAKAYA KIKWETE na Mkewe walikuwa mstari wa mbele kuhamasisha watanzania kupima afya zao.
Rais JAKAYA KIKWETE akilia kwa uchungu siku alipokuwa akiuaga mwili wa Marehemu Komba, pembeni yake ni Anne MAKINDA
Rais JAKAYA KIKWETE na mkewe wakiwatia moyo familia hii
Watoto wengi walimpenda Rais wao ambae hivi karibuni ataiachia nchi kwa Rais Mpya wa TANZANIA.
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ambae mara baada ya wiki ijayo atakabidhi kwa Rais mpya wa Tanzania baada ya kumaliza majukumu yake ya kuingoza nchi hii mika kumi kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi kuwa kila baada ya miaka kumi lazima wabadilishe Rais mwingine.
Hata hivyo Rais Jakaya Mrisho Kikwete atakumbukwa kwa mengi mazuri ambapo watanzania wengi watamkumbuka kwa uchangamfu wake tabasamu lake licha ya kwamba alikuwa kiongozi wa Taifa lakini hakuwa mbali na wananchi wake kwa kupiga nao stori kujadiliana mambo mbalimbali.
Rais sasa anakwenda kuungana na team ya marais waliotangulia kama Mkapa, Mwinyi na atakuwa kama raia maarufu akama yeye mwenyewe anvyosema, licha ya kwamba anakiachia kiti cha urais lakini atakuwa anaonekana kwenye majukumu mengine ya kitaifa kama tunavyowaona marais wastaafu.
Hata hivyo kuna mambo kumi ambayo watanzania watamkumbuka Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwemo mkewe Mama Salma Kikwete.
Alikuwa na upendo mkubwa kwa Watanzania wote bila kujari itikadi zao.
Kila palipotokea matatizo ya msiba, ama majanga yoyote lazima auhudhurie akiambatana na mkewe. na mengineo mengi. Tunamtakia mapunziko mema Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE.
No comments:
Post a Comment