FILAMU YA WAKE UP YA MSANII MANAIKI SANGA AMBAY MWISHO WA MWEZI HUU ITAKUWA MTAANI KWA MAELEZO ZAIDI MCHEKI KWENYE Manaiki Sanga instagram utapata mengi zaidi kuhusu movie hiyo
Ernest Napoleon staa wa filamu ya Going Bongo
Na Ripota maskanibongotz Uingereza
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida siri nzito imevuja kuhusu shoo anazozifanya
nje ya nchi msanii Diamond hasa nchini Uingereza na kubainika kuwa kumbe
mwanamuziki huyo hufanya maonesho yake sehemu yenye hadhi ya chini na
inayokaliwa na watu masikini kupita kiasi.
Habari
za uhakika toka kwa Raia mmoja toka nchini Kenya aliyejitambulisha kwa
jina la Otieno ambae pia mshirika kwa moja ya kampuni za mapromota
wanawaandalia shoo wasanii wa Afrika Mashariki na Kati ambae anaishi
nchini Uingereza alisema" Unajua tatizo la wanamuziki wa Tanzania ni
kuficha ukweli wa mambo mara nyingi huwa nasikia wakitamba kuwa wao ni
wa kimataifa na shoo zao za kimataifa awa wapi hiyo sio kweli mafano
mzuri ni onesho la Diamond alilolifa tarehe 16 may, 2015.
Otieno
aliendelea kusema katika onesho hilo Diamond alilifanya katika eneo la
East London eneo ambalo hukaliwa na watu masikini na wenye hadhi ya
chini na hata kiingilio chao huwa ni kidogo sana " Kwa wanaojiua
Uingereza watakuwa wanailijua eneo hili kiukweli ni eneo ambalo wasanii
wengi wanaoitwa wenye hadhi ya chini ndiyo hutupwa huk, lakini kumekuwa
na uposhwaji na sijui ni promo au nini utakuta msanii anapopata nafasi
ya kupelekwa huko basi katika nchi yake hutangaza kuwa anakwenda kufanya
shoo Uingereza bila kutaja eneo analokwenda kufanya onesho lake yeye
anachong'ang'ania ni Uingereza ili watu watishike na kumuona wa matawi
ya juu" Alisema Promota huyo
Promota
huyo aliongeza kusema Diamond hajulikani hata kidogo nchini Uingereza
ndiyo maana hata hutupwa huko polini na ili kuona kama hajulikana
wanaokuja kuhudhuria onesho lake ni watanzania wachache tu ambao
hawazidi hata elfu 20 na huwezi kukuta mastaa wakubwa wanashiriki onesho
lake kutokana na kutomtambua na kushindwa kufahamu anachokiimba
mwanamuziki huyo.
Habari
zaidi zilielezwa kuwa wasanii wenye ubavu wa kufanya onesho katika ya
mji wa Uingereza ni kama Davido, Jose Chamilioni, P-Square na wengineo
na sababu kubwa ya wasanii hao kufanya maonesho hayo katikati ya mji ni
kutokana na Wanigeria wengi kuishi katikati ya mji ambapo ilikadilikiwa
wanigeria zaidi ya laki mbili wanaishi katikati ya mji hali, lakini pia
kutokana na kazi zao kujulikana kimataifa kuliko za Diamond.
Hata
hivyo mkenya huyo alisikitishwa na tukio la Diamond la kumfanyia umafia
msanii mwenzake aishie nchini Marekani aliyefika kwenye onesho lake kwa
ajili ya kuonesha trailer ya filamu yake iitwayo Going Bongo.
Otieno
alisema kuwa Ernest Napoleon ambae ni msanii wa Kitanzania na ndiye
staa wa filamu ya Going Bongo aliongea na promota wa Bongo Deejays
walio-organize concert hiyo kuonyesha trailer ya Going Bongo kabla ya
Diamond kupanda jukwaani. Ernest Napoleon alilipia projector pamoja na
hela ya kuonyesha trailer yake.
Mkenya aliongeza kusema Trailer hiyo ilijaribiwa kabla ya shughuli hiyo kuanza, na kutokuwa na hitilafu yeyote kwa upande wa
picha au sauti. Lakini baada ya Ernest Napoleon kupanda jukwaani na kumtangaza Diamond pamoja
na movie yake ya Going Bongo, deejay wa Diamond aliingia ghafla kwenye mitambo na kuondoa sauti ya
trailer.
Wakati huo huo Diamond alipelekewa Mic backstage na kuanza kuimba wakati trailer hiyo ikionyeshwa.
Ernest Napoleon alishuka kwenye stage kufuatilia kwa nini trailer inaonyeshwa bila sauti, Diamond aliingia stejini na kuanza kutumbuiza huku trailer hiyo ikimuulika kifuani mwake hali ilionesha Diamond aliamua kumfanyia umafia msanii huyo.
Kilichofuatia ni mvutano kati ya Ernest Napoleon na team ya Diamond kuhusu hitilafu ambazo hazikuonekana kabla ya trailer hiyo kuonyeshwa. Promota wa event hiyo baada ya majadiliano ya muda mrefu na kwa shingo upande walirejesha pesa waliyopewa ingawa hawakulipia projector ambayo ililetwa special kwa ajili ya kuonyesha Going Bongo.
Wiki kadhaa baada ya onyesha la Diamond ambalo lilifanyika eneo la East London ambapo wasanii wengi wa Bongo hufanya matamasha yao kutokana na bei nafuu ya eneo hilo ambalo linakaliwa na watu wenye kipato cha chini mjini, London, Going Bongo ilizinduliwa West London katika eneo ambalo movie au show za muziki kutoka Afrika hazifanyiki kwa sana.

Uzinduzi
wa Going Bongo ulihudhuriwa na mastaa wa Uingereza wakiwemo wa jumba la
Big Brother Uingereza, Akia Katobe wa Mad Men, Sean Cronin wa Mission
Impossible, Grace Andrews wa Towie, Ella Jade wa Apprentice na wengineo
wengi. Uzinduzi huo uliandikwa na media nyingi kubwa za Uingereza
zikiwemo Daily Mail
Kitendo
hicho kilionekana kumkera mkenya huo na kupelekea kumdharau mwanamuziki
huyo kwa roho ya kiswahili aliyomfanyia mtanzania mwenzake.
Gazeti
hili lilipomtafuta sataa wa filamu ya Going Bongo Ernest Napoleon ili
kuthitibisha taarifa alikiri ni kweli kulikuwa kumetokea tukio hilo
dhidi yake kutoka kwa Mwanamuziki huyo lakini alishasamehe muda mrefu na
ndiyo maana ni tukio la toka mwezi wa tano lakini yeye hakuwahi kusema
lakini kiukweli tukio hilo liliwashtua hata raia wa Tanzania waishio
nchini Uingereza.
Upande
wa Diamond alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani ili aweze
kuzungumzia tukio hilo simu yake haikupokelewa licha ya kugigwa zaidi ya
mara sita hadi gazeti hili linaenda mitamboni.
Source: maskanibongotz
No comments:
Post a Comment