TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, October 18, 2014

MAHAKAMA YAMPIGA STOP DAVIDO KUFANYA ONESHO LA FIESTA YA LEO. MASHABIKI WASEMA PRIME PROMOTION NA CLOUDS FM VIPOTEZA SIFA

 Hii ndiyo taarifa ya Mahakama iliyotolewa jana ya kumzuia Davido kutofanya onesho lolote la Prime Promotion kwani tayari alikuwa keshaingia mkataba na kituo cha Radio Times mkataba wa kufanya onesho hilo
 Mwanamuziki Davido akishangaa mara baada ya kupokea taarifa za kuzuiwa kufanya onesho lake kwenye jukwaa la Fiesta leo hii Jumamosi kwenye viwanja vya Leaders Club.
Hivi ndivyo maandalizi ya jukwaa la Fiesta lilivyokuwa linaendelea na sijui hadi sasa hali ikoje.
Na Sakina Shabani
Kweli waliosema mwisho wa ubaya ni aibu waliona mbali sana hivyo ndiyo kituo cha Clouds Fm Radio & Prime Prodution walivyoanza kujishushia hadhi walijijengea miaka mingi nchini baada ya kumrubuni msanii toka Nigeria Davido kuja kufanya shoo kwenye onesho la Fiesta wakati tayari alishaanza kusikika kwenye kituo cha radio Times Fm 100.5 kwa jingo kama atakuwepo Tanzania Nove 1. 2014.
Katika sakata hilo mashabiki wa kituo hicho cha Clouds Fm wameongea mengi  na kutoa ushauri kwa viongozi wa kituo hicho, ambapo Jackline Mushi mkazi wa Ukonga Jijini Dar alikuwa na haya ya kusema " Kiukweli Clouds kwa hili wamejidhalilisha walishindwa kuandaa msanii wao hadi wamdandie msanii ambae tayari ameshaingia mkataba na kituo kingine hadi Mahakama inaiingilia kati hii ni aibu kwa kampuni kama hiyo yenye uwezo mkubwa sana" Alisema msichana huyo
Aidha nae Edwini Chiwanga ambae ni Polisi Kilwa Road alikuwa alisema" Kweli mwisho wa ubaya ni aibu Clouds iliheshimika sana miaka mingi lakini  kwa uletaji wasanii lakini naona sasa imeshaanza kupoteza sifa Mungu amewaumbua" Alisema
Maoni yalikuwa mengi sana lakini hata hivyo na wako ambao waliomba hifadhi ya majina yao walisema kuwa kituo hicho cha Clouds sasa kinatakiwa kukubali chalenji kwenye uandaji matamasha Times ni kampuni ya kitanzania tena na Clouds pia hivyo ni vyema kushirikiana kwenye masuala hayo ya burudani ili kuleta sifa njema kwa nchi yetu kuliko kutaka kukomoana na mwisho ni aibu kama hizi Mahakama sasa imetoa amri hiyo na sijui itakuaje.

No comments:

Post a Comment