TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, June 25, 2014

UAMUZI WA KOCHA WA ITALIA BAADA YA TIMU YAKE KUSAMBARATISHWA NJE YA KOMBE LA DUNIA NI HUU HAPA..!



Muda mchache baada ya timu yake kuondolewa rasmi kwenye michuano ya kombe la dunia kwa kushindwa kufanya vyema katika mechi za makundi kwa mara ya pili mfululizo katika kombe la dunia, kocha Cesar Prandelli amefanya maamuzi magumu.
Italia iliondolewa baada ya kufungwa kwa goli 1-0 na Uruguay katika mechi ya mwisho ya makundi.
Baada ya mchezo Prandelli akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari alitangaza kujiuzulu kuifundisha timu hiyo.
“Nilichagua mfumo fulani wa ukufunzi na ndio sababu ninajiuzulu, kwa sababu haukufanya kazi,” alisema.
Aliongezea: “Kuna jambo ambalo limebadilika tangu nilipotia saini mkataba mpya. Sijui kwanini lakini sina haja ya kutafuta sababu .”
Kocha huyo aliingia mkataba mpya na Italy Mei mwaka huu ambao ungemfanya aendelee kuifundisha Italy hadi baada ya mashindano ya kuwania ubingwa wa Euro ya mwaka wa 2016.
Prandeli amechukua hatua hii baada ya kujiuzulu kwaa rais wa shirikisho la kandanda la Italia Giancarlo Abete.
“Nilizungumza na rais wa shirikisho na naibu wa rais Demetrio Albertini na nikawapa barua ya kujiuzulu kwangu. Ni jambo lisilobadilika,”

No comments:

Post a Comment