TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, June 17, 2014

MMH MWANAFUNZI HUYU AVUA NGUO MBELE YA WAHESHIMIWA NA KUWAJAMBIA, ASEMA ILIKUWA NI FURAHA BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAKE NI AIBU KUBWA AISEE..!




Wasomi wanapokutana hasa katika zoezi la kutunukiwa cheti kama kielezo cha uhitimu wa ngazi fulani kuna vitu huwezi kuvifikiria kama vitatokea hata kidogo.
Katika Jack Britt High School, North Carolina, Marekani wanafunzi mmoja amewaacha hoi mamia ya watu waliohudhuria sherehe ya kutunukiwa vyeti (graduation) baada ya kupanda jukwaani kupokea cheti chake na ghafla akavua johon lake na kubaki na boxer.
Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote miwili juu kama mwanamieleka anayetamba. Lakini haikuchukua round wanausalama wakamdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo alinyang’anywa diploma yake na hivyo hakukabithiwa cheti.
Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa hana kielelezo cha elimu yake.
“Shule yetu imefanya jitihada kubwa. Hapo zamani watu waliohudhuria walikuwa wenye vurugu wakati wa graduation. Tumefanya jitihanda kuwafanya watu waheshimu wanafunzi. Huyu kijana amechagua kutoonesha heshima kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank Till, mwalimu wa chuo hicho.
 

No comments:

Post a Comment