TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, June 26, 2014

HATIMAE KOCHA MPYA WA YOUNG AFRICANS ATUA JIJINI DAR


Kocha mpya wa Yanga SC, Marcio Maximo baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.


Kocha Marcio Maximo ametua jijini Dar muda mfupi uliopita kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kuanza kuifundisha timu ya Yanga. Maximo amepokelewa kwa shangwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na mashabiki wa Yanga. Aidha kocha huyo amesaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo kwa miaka miwili
JUMLA ya shilingi milioni 371 zimetumika kuhakikisha kocha huyo ametua Jangwani.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ndiye aliebeba jukumu hilo la kumwaga mamilioni hayo ya fedha ili kumpata Maximo, kocha wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars.Mbrazili huyo aliwahi kuifundisha timu ya taifa, Taifa Stars kabla ya nafasi hiyo kutua kwa Mholanzi, Jan Poulsen aliyeondolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, kamati ya utendaji ya timu hiyo ilikutana hivi karibuni na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo la usajili na suala la kocha.Chanzo hicho kilisema, katika kikao hicho, viongozi hao wamempendekeza Maximo kuja kukinoa kikosi hicho kwenye msimu ujao wa 2014-2015. Jambo ambalo wamelitekeleza leo kwa kocha huyo kuwasili nchini.

Kilisema kuwa, kocha huyo amekubali kuja kuifundisha Yanga kwa mshahara wa dola 16,000 (sawa na shilingi milioni 25) kwa mwezi, hivyo kwa mwaka mmoja timu hiyo itamlipa Mbrazili huyo shilingi milioni 307).
Kiliongeza kuwa, pia kocha huyo anataka fedha ya uhamisho dola 40,000 (sawa na shilingi milioni 64), hivyo jumla ya fedha watakazotumia Yanga ni shilingi 371.
“Fedha hizo ndizo tumefikia hapo, lakini bado kuna majadiliano kuhusiana na kupunguza kiwango cha mshahara na fedha za kusaini. Halafu litakuwa ni suala la Maximo atakuja lini nchini,” kilieleza chanzo.

Pamoja na juhudi hizo za Manji kumleta Maximo, kumeibuka mkanganyiko kuhusiana na kipa wa Yanga, Juma Kaseja ambaye alikuwa hana uelewano mzuri ma Maximo.

Wakati akiwa Stars, Maximo aliapa kutomuita Kaseja katika kikosi chake licha ya kwamba alikuwa ndiye kipa bora nchini na namba moja katika kikosi cha Simba.
Maximo alidiriki kumuita Ally Mustapha ‘Barthez’ ambaye hakuwa amedaka hata mechi moja Simba, hali iliyozua mkanganyiko na kamwe hakuwahi kusema tatizo lake na Kaseja ni lipi.“Kweli kuna mpango wa kuanza ufumbuzi kuhusiana na suala la Kaseja. Wote wanahitajika Yanga, hivyo kutakuwa na mjadala kuhusu hilo na lengo ni kuona wanafanya kazi pamoja,” kilieleza chanzo.
“Tutamtaarifu Maximo na kumueleza hali halisi, tunaamini hakutakuwa na tatizo.”


Manji aliwaeleza jana wanachama wa Yanga kwamba kamati ya utendaji imefikia uamuzi wa kumleta kocha huyo ingawa dalili zilionesha kuwa jambo hilo lina uhakika wa asilimia 90.
“Juzi usiku tulikutana kamati ya utendaji kufikia muafaka wa kumleta Maximo, hivyo kila kitu kinakwenda sawa, vipo baadhi ya vitu tunavikamilisha,” alisema Manji wakati akizungumza na wanachama.

No comments:

Post a Comment