Mwenyekiti wa Azam FC mzee Said Mohamed Said
Na Livingstone Mkoi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua blog
hii pendwa ya Maskanibongotz imenasa taarifa juu
ya maofisa wa timu ya Azam wanavyomuwinda mchezaji
wa kimataifa wa Yanga Mbuyu Twite ili ajiunge na
timu hiyo.
Habari za uhakika toka ndani ya familia ya
mchezaji zilizothibitishwa na mdogo wake na
mchezaji huyo aliyefahamika kwa jina la Erick
zilisema kuwa maofisa hao wa Azam wamekuwa
wakimuwinda mchezaji huyo usiku na mchana ili
wamsainishe.
Akiongea na mwandishi wetu mdogo huyo Twite
alisema" Kaka mashabiki wa Yanga wasiwe na shaka
kwani Twite ni mtu mwenye msimamo hao maafisa wa
Azam wanamsumbua sana hata jana wamekuja usiku
wakimtaka asaini wakiwa na fuko limejaa pesa dola
lakini tuliwatimulia mbali" Alisema Erick
Hata hivyo Erick aliongeza kusema" Kama haitoshi
juzi walituma mwandishi wao ambae alikuja kwa gia
ya kumuhoji Twite lakini akaleta dola mia saba
akidai ni za soda tu" Alisema kijana huyo ambae
nae ni mchezaji anaewaniwa na timu ya Mbeya City
Maskanibongotz.iliwasiliana na msemaji wa timu ya
Azam yenye makao yake makuu Chamanzi Jijini lakini
kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana.
SOURCE: Maskanibongotz
No comments:
Post a Comment