TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, May 28, 2014

JESHI LA POLISI LATANGAZA KIAMA KWA WATOTO WA MBWA, MSAKO WA MTAA HADI MTAA UMEANZA JANA MAENEO YA YOTE YA JIJI LA DAR..!


Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa
 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu au Panya Road.  Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.
 Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk.  Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia
Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita

No comments:

Post a Comment