BAADA ya kutokea kwa sintofahamu ndani ya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kwa wabunge wanaounda umoja wa Ukawa
kutoka nje, wengi wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kukivunja chombo hicho.
Tivoli Athuman, mkazi wa Mwenge jijini Dar, alisema ni bora Rais akalivunja bunge hilo kwa vile wajumbe wake wameonyesha udhaifu mkubwa wa kushindwa kutetea hoja zenye masilahi kwa wananchi, badala yake wameweka mbele utashi wao binafsi na vyama vyao.
“Wote tunajua kwamba kinachotafutwa pale ni katiba ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ni jambo la ajabu kuona wajumbe wanafika pale na kutanguliza misimamo yao na vyama vyao utafikiri ndicho walichotumwa na wananchi, mimi nafikiri JK angelivunjilia mbali bunge hili,” alisema.
Mwanamtwa Palango wa Kurasini, alimlaumu Rais Kikwete kwa kuwajumuisha wabunge kwenye bunge hilo maalum, kwani wao ndiyo chanzo cha kukwamisha mambo mengi ya msingi kupata katiba mpya.
“Hakukuwa na sababu ya kuwajumuisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
tumeshawaona hawa ni watu wa malumbano tokea mwanzo, kuwaleta huku ni kuvuruga mambo tu, hapa ilibidi Rais ateue mwenyewe wajumbe wasio wanasiasa.“Hakukuwa na sababu ya kuwajumuisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
No comments:
Post a Comment