TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, March 3, 2014

MH: JANUARI MAKAMBA AWAPA SHAVU NENE WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI, AWAITA DODOMA HARAKA SANA, MESSI CHENGULA AFUNIKA KWENYE UZINDUZI WAKE..!

 Mtangazaji wa DTV, CTN  ELISHA ODADA akifanya mahojiano na BAHATI BUKUKU aliyefika kwenye uzinduzi wa albamu ya Mungu Habadiliki ya mwanamuziki Messi Changula jana kwenye Hoteli ya Ubungo Plaza.
 Mh. January Makamba akiwa na familia yake mkewe na wanae wakishuhudia uzinduzi huo wa albamu ya Messi Changula Mungu Habadiliki.

 Messi Changula kulia akiwa Hightable na wageni waalikwa muda mfupi kabla ya kuzindua albamu yake.


 Mtangazaji wa Wapo Radio kushoto Ritha Chiwalo kushoto, katikati ni mwanamuziki Neema Gaspa wakifurahia jambo kwenye hekaheka za uzinduzi huo uliofana kinoma.



 Watumishi wa Mungu wakiombea CD hizo kabla ya kuzinduliwa na Mh Januari Makamba.


 Rose Muhando akifanya balaa kwenye uzinduzi huo.
Mh Makamba akimpongeza Rose Muhando.
Na Sakina Shabani.
Ule Uzinduzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa injili sasa umefanyika na kufana ile mbaya.
Uzinduzi huo ulifanyika jana kwenye ukumbi wa Hotel  ya Ubungo Plaza na kushuhudiwa na maelfu ya wananchi wakiongozwa na Mh Januari Makamba aliyefika na familia yake kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Xdeejayz ambayo ilikuwepo uwanjani ilishuhudia mambo makuu kadhaa ya kushangaza ambayo huenda hayajawahi kutokea kwani nyota ya mwanamuziki huyo ni kubwa sana wanamuziki wenzake karibia wote walifika kumsapoti kwwenye uzinduzi huo.
Hali hiyo ilimpa faraja kubwa mwanamuziki huyo aliyekuwa anazindua albamu yake iitwayo Mungu Habadiriki na kumfanya mgeni rasmi Mh January Makamba kushangazwa na umati mkubwa wa watu waliohudhuria na kutoa ahadi ya kushirikiana pamoja na wanamuziki hao ambao kwa sasa wanampango wa kuanzisha chama cha muziki wa injili Tanzania.
Hata hivyo Mh Makamba alianza kuizindua albamu hiyo kwa kutoa shilingi milioni moja kisha akafuatia mkewe na familia yake. Hata hvyo jambo kuu alilosisitiza Makamba ni jinsi wanamuziki hao wanavyotakiwa kushirikiana na kujiandikisha kwenye chama hicho ili kiwe msaada kwao pale inapotokea tatizo kwa mwanamuziki mwanachama.
Nae Messi aliiambia Xdeejayz kuwa anamshukuru Mungu kwa neema aliyompa kwani kujitolea kwa wanamuziki wenzake kuja kumsindikiza ni jambp la faraja na ni neema kwa Mungu tu si vinginevyo.
 Albam hiyo ambayo kwa sasa inapatikana madukani kote na siku mbili hizo itawafikia watu wa mikoani hivyo wakae mkao wa kula kuchuka cd orijino.
" XTREME DEEJAYZ WANAKUJA KUWASHIKA IJUMAA HII UKIKOSA SHOW HII HAKINA HAUTOPATA WA KUKUELEZA KILICHOTOKE NI NDI YA CLUB MAISHA DAR"

No comments:

Post a Comment