NI MVUNGI?
NI BAHATI BUKUKU?
NI CHRISTANA SHUSHO?
NI UPENDO NKONE?
Alex Msama ambae amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wasanii wa Injili, lakini amelalamikiwa kushindwa kunusuru hali mbaya ya wasanii hao wanaotoka nje ya imani na kutumia madawa ya kulevya.
Mchunga Kiongozi Mama Rwekatare
Na Mwandishi WA Xdeejayz
Hali si shwari kwenye tasnia ya muziki wa injili Tanzania kufuatia baadhi ya waimbaji wake kuanza kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo za kutumia madawa ya kulevya pamoja na ulevi.
Gazeti la Maskani Bongo pamoja na Blog hii mahili kwa habari za uchunguzi inaendelea kuingia chimbo kwa ajili ya ukusanyaji data za wasanii wote wanadaiwa kunywa pombe na wanaotumia madawa ya kulevya ili kuwaanika hadharani ili jamii inawafahamu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu toka ndani ya tasnia hiyo ambae aliomba hifadhi ya jina lake na kusema kwa sasa hali si swali kutokana na wanaumuziki hao kwenda kinyume na maandiko ya Mungu kwani wako wanaoingia stejini wakiwa wamezimua viroba, wako wanajidunga sindano za madawa ya kulevya na wengine wanakunwa pombe kabisa hali inayoondoa maana halisi ya neno ulokole.
Hata hivyo wakati mapaparazi wetu wako msituni kukusanya diteizi mashabiki mbalimbali wameanza kupoteza imani hata ya kuhudhuria matamasha ya injili yatakayotarajia kufanyika hivi karibuni kwani hawezi kuwenda kuangalia injili ya uimbaji kwa watu walevi watumia madawa ya kuleva nk.
Aidha mashabiki hao waliendelea kusema kuwa uimbaji ni sawa na kuhubiri injili lakini hivyo waimbaji wote hawana tofauti na wachungaji kwani wote hufanya kazi moja ya kutumkia mungu tofauti ni kwamba huyu anamtumika kwa njia ya uimbaji huyu anamtumikia kwa njia ya kuhuburi
Hata hivyo mashabiki wengi wamesikitishwa na jinsi Mtumiishi wa Mungu Alex Msma jinsi alivyoshindwa kuwasaidia wasanii hao kwani licha ya kwamba amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia kuhusu kazi zao pia angewasaidia pia wapotee kwenye dhambi ya ulevi na utumiaji madawa ya kulevya. Hivyo wamemuomba kwa kuwasaidia wasanii hao wasitumie madawa na ulevi ili mashabiki warudishe imani yao kwao inayoendelea kupotea na asaidiane na watumishi wengine wa Mungu ili wawasaidie wasanii hao.
Blog hii na Gazeti la Maskani Bongo likishakamilisha uchunguzi huo litawaanika hewani wanamuziki wote nyota wanaokumbwa na kashfa hizo mbaya za madawa ya kulevya.
"KWA HABARI ZAIDI USIKOSE GAZETI LAKO NAMBA MOJA TANZANIA LA MASKANI BONGO JUMATANO LITAKUWA NA HABARI KAMILI"
No comments:
Post a Comment