Siku moja baada ya wimbo mpya wa Ommy Dimpoz "Miss koi koi" kuvuja
kwenye mtandao, Ommy Dimpoz amlalamikia producer "Manecke" kutoka AM
Records na kudai yeye ndio atakuwa kaivujisha
"hiyo nyimbo wakati wa tuzo za kilimanjaro ambazo nilipata awards zangu
za kwanza za song ya Nainai, ndio kipindi ambacho katika wiki hiyohiyo
nilikutana na Manecke na tuka plan kufanya kitu, i think ilikuwa ni
2012, nikaenda nikarecord nyimbo... unajua kama msanii unakuwa kila siku
una record unarecord lakini baadae unaangalia labda planning nyimbo gani
intoke, kwahiyo ilikuwa ina muda kidogo, hebu fikiria mpaka nimekuja
kutoa baadae me and you, tupogo na nilikuwaga sijawahi hata kuzirecord
hiyo nyimbo ilikuwa tayari nimeshairecord."
"Mimi sasa nikaaamua jana kuidownload ile nyimbo na nilivyoicha studio
niliiacha kama demo, lakini nilivyoi download naona kabisa kama ni
nyimbo imeshamaliziwa kwa kiasi flani kwa kule mwisho, kwahiyo nikama
nyimbo imeshafanyiwa mixing halafu mtu akaitoa, sasa kama mimi nimeacha
nyimbo studio unategemea kwamba anaeitoa ile nyimbo ni nani? ni
producer, huwezi ukasema labda aaaaaaah wanatoa wenyewe, mimi sikuwepo
sikuwa na ile nyimbo! nimeitoa vipi sasa?."
Je aliongea na Manecke baada ya kusikia wimbo huo?
"ki ukweli hii ni kazi yangu na mimi ndio ninaitegemea, kwamba
ninavyofanya kitu flani nakua na mipango nacho, kwahiyo hata kama
ningekuwa nataka kufanya hata hiyo nyimbo ningetaka iwe kubwa, ina maana
ningetengenezea mipango iwe kubwa, lakini nimesikitika kiasi kwamba
nimeshindwa hata kumpigia Maneke, sababu kama kitu kimeenda kwenye
mitandao nikaona nami ni bora niandike kwenye twitter yangu kuwa
Sija-release nyimbo yoyote tangu nilipotoa tupogo, lakini kuna nyimbo
nimefanya miaka miwili iliyopita katika studio za AM reacord chini
Maneke, na kama inavyolalamikiwa na wasanii wengine kuwa nyimbo zinavuja
kutoka kwenye studio hiyo na nyimbo yangu pia imevuja."
"GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI KILA JUMATANO PATA KOPI YAKO"
No comments:
Post a Comment