MCAMEROON
Samuel Eto’o amelichangamsha Jiji la London leo baada ya kufunga mabao
yote matatu katika ushindi wa 3-1 wa Chelsea dhidi ya Manchester United,
Uwanja wa Stamford Bridge.
Eto’o
alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza dakika ya 17 na 45 na baadaye
dakika ya nne tangu kuanza kipindi cha pili akakamilisha hattrick yake
kabla ya kumpisha Fernando Torres dakika ya 79.
Javier
Hernandez ‘Chicharito’ aliyetokea benchi dakika ya 56 kuchukua nafasi
ya Ashley Young aliwafungia Mashetani Wekundu bao la kufutia machozi
dakika ya 78.
Nemanja Vidic alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei na Man United ikaishiwa nguvu kabisa.
Ushindi
huo, unaifanya The Blues ya Jose Mourinho ifikishe pointi 49 baada ya
kucheza mechi 22, ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City
pointi 50 na Arsenal pointi 51, wakati United ya David Moyes inabaki
nafasi ya saba pointi 37.
Samuel Eto’o akishangilia moja kati ya mabao yake aliyofunga kwenye Uwanja wa Stamford Bridge leo
Katika
mchezo uliotangulia, Tottenham Hotspur imeifunga Swansea City mabao 3-1
nyumbani kwake. Mabao ya Spurs yalifungwa na Emmanuel Adebayor dakika
ya 35 na 71 na Chico aliyejifunga dakika 53, wakati la wenyeji la
kufutia machozi lilifungwa na Bony dakika ya 78.
"GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI JUMATANO WIKI HII LIKIWA NA HABARI MOTO MOTO"
No comments:
Post a Comment