Na Sakina Shabani
Kituo cha runinga cha Dar es salaam Televisheni DTV kimevunja
rekodi kwa kuandaa tamasha kubwa la waimbaji wa nyimbo za Injili linalotarajia
kuifanyika mapema mwezi desemba mwaka huu.
Akiongea na gazeti hili mratibu wa tamasha hilo Mathew
Philip ambae pia ndiye meneja wa kituo hicho cha maarufu cha runinga alisema “
Ni hivyo tumejipanga kufanya uzinduzi wa kipindi chetu kipya cha SIFA ZA
USHINDI kinachorushwa kila siku za Jumapili ndani ya DTV” Alisema meneja huyo
Aidha Meneja huyo aliendelea kueleza kuwa katika uzinduzi huo wamealikwa wanamuziki
zaidi ya sabini toka ndani na nje ya nchi kuja kuhudhuria kwenye uzinduzi huo
pamoja na kutoa burudani kwa mashabiki.
Mathew Philip aliongeza kusema kuwa licha ya kwamba tamasha hilo ni
la uzinduzi wa kipindi hicho pamoja na uimbaji pia watakuwa na maombo maalum ya
kuimbea amani nchi yetu bila kujali itikadi za watu wote. Na wapenzi wa nyimbo
za injili wakae mkao wa kula kwani tamasha hilo litakuwa ni la kipekee huenda
likawa moja ya matamsha makubwa na yatakayofanya viuzri nchini.
Meneja
huyo aliwataja waimbaji hao ambao ni baadhi tu kuwa ni Bahati Bukuk ,Boni
Mwaitege, Edson Mwasabwita, Happy kamili, Flora mbasha, Madam Ruti, Neema
gasper, Matha Baraka, Siza mwampamba, Prisca Mwalugaja, Elizabeth Nzunda, Davdi
Robert, Adelina Swai, Jackline Falles, Sara Mvungi, Victor Aron, Danny Bandezu,
Dar gospel, Kwaya ya cvc chang’ombe na wengineo wetu.
Mratibu
huyo
aliongeza kusema tamasha hilo litafanyika Desemba 8 kwenye viwanja vya
Ustawi wa Jamii huku kiingilio kikiwa elfu tano kwa wakubwa na elfu
mbili kwa watoto!
"GAZETI LA MASKANI BONGO LITAKUWA MTAANI KUANZIA DESEMBA KAA MKAO WA KULA!!!"
No comments:
Post a Comment