TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, November 8, 2013

MWANAMUZIKI OMARI MKALI YAMKUTA MAKUBWA, HOFU YA KUTENGWA NA WAISLAMU YAFUKUTA SOMA KILICHOMTOKEA!


 Mwanamuziki Omar Mkali akiwa kwenye gari yake leo baada ya kupata kashkash msikitini kufuatia taarifa zilizoandikwa  kuwa sasa hivi amejiingiza kwenye muziki wa Injili kwa kumtumikia Mungu kupita uimbaji!
 Na Sakina Shabani
Mwanamuzki mkongwe nchini ambae amewahi kutamba sana miaka ya nyuma wa uhai wa bendi ya Pamo Sound Omari Mkali amekubwa na mazito kufuatia gazeti moja linalotoka mara 2 kwa wiki kulipoti kuwa sasa hivi ameachana na imani aliyokuwa nayo na anaimba kwaya.

Omari alisema taarifa hizo zimempatia usumbufu mkubwa sana kwa watu wa imani yake kiasi cha kumfanya kuhofia kukanyaga msikitini akihofia kipigo au kutengwa na waumini wenzake" Kaka imenisikitisha sana kuona habari hiyo kwani sio kweli kwamba mimi nimeachana na imani yangu hapana mimi bado ni mtoto wa kiislamu na kila siku iendayo kwa mungu naenda kuswali msikitini" Alisema Omar

Aidha Omari aliongeza kusema kuwa kilichomponza hadi yakamkuta hayo ni jinsi anavyofanya kazi na waimbaji wa nyimbo za dini" Unajua watu wanashidwa kutambua kuwa mimi ni prodyuza na huwa nawatengenezea nyimbo waimbaji hao wa Injili na hata kuwasaidia kidogo kuwaingizia sauti hivyo hali hiyo imekuwa tatizo kwangu na watu kutafsiri huenda mimi nikawa nimeokoka jambo ambalo sio kweli" Alisema

No comments:

Post a Comment