TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, October 15, 2013

SHEKH SHARIF ALIYEPATA AJALI HALI YAKE YABADILIKA GHAFRA, WATANZANIA WATAKIWA KUMUOMBEA DUA APONE HARAKA!


Kijana shekh sharif Khamis “16” ambae amekuwa kwenye kalama kubwa za mwenyezi mungu kwa dua zake katika ya wiki hii amenusika kifo baada gari yake kupata ajali mbaya kupelekea kuzunguka zaidi ya mara tatu na hali yake sio nzuri kutokana na kuumia nyonga ya mguu wa kushoto.
Akiongea kwa shida kwa njia ya simu namba 0717-688792 Shekh sharif alisema kuwa ajali hiyo iliwapata wakati wakitokea kijiji cha Mwailanje kuelekea Kiteto Mkoani Arusha na wakiwa wanaelekea kwenye majukumu ya kiimani huku gari hiyo ikiendeshwa na ustaadh Seif Othman na bila kutarajia alitokea mtoto akiwa anaendesha baiskeli kwa kasi mbele yao na dereva alipoona mtoto huyo anakaribia kuivaa gari kwa mbele ndipo alipomkwepa.
Hata hivyo Shekh huyo aliongeza kusema baada ya dereva wake kufanikiwa kumkwepa Yule mtoto  ghafra upande uleule aliokwepea upande wa kushoto tairi la mbele lilipasuka upande ambao alikua amekaa shekhe huyo.
Baada ya kupasuka tairi hilo gari hiyo lenye namba za usajili  T283  AJZ aina ya  Lexus Aristi ilipoteza muelekeo na kupinduka zaidi ya ya mara tatu kama inavyoonekana kwenye picha ambapo baada ya hapo watu wote waliokuwemo ndani yake walitoka walipatwa na mshutuko huku shekh sharif mwenyewe akiuumia vibaya.
Akiongea mara baada ya ajali hiyo shekh huyo ambae amekuwa nchini na bara la afrika kwa ujumla kutokana mihadhara yake ya kuwaombea dua watu na kabla ya kuelekea mkoani Arusha shekh huyo alikuwa kwenye ziara za nchi za Burundi, Kongo, Angora na Zambia ambako huko alifanya mambo ya kushangaza kwa dua zake kuziombea amani nchi hizo zenye migogoro ya kivita.
Aidha katika hatua nyingine Shekh huyo mwanzoni mwa mwaka jana aliwahi kupata ajali nyingine kama hiyo ambayo gari yake ilitumbukia kwenye korongo na kukunjika kunjika kama chapati maeneo ya Morogoro lakini kwa kudra za mwenyezi mungu alitoka salama.

No comments:

Post a Comment