TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, September 27, 2013

MSANII HUYU WA BONGO MOVIE KUNA SIKU WATAKUJA KUMBAKA HADHARANI KWA MAVAZI YAKE YA NUSU UCHI, APEWA ANGALIZO!!!

 
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amejikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa kutokana na kukatiza kitaa akiwa na nguo iliyombana na kuonesha makalio yake yaliyojazia.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, tukio hilo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita maeneo ya Mwenge, jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa ameenda kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali ndipo kundi la wanaume wakware lilipoanza kumzomea.

Tukio hilo lilimfanya Amanda apoteze amani ghafla na kuamua kutimka zake eneo hilo huku akiwashangaa. Paparazi wetu hakuwa nyuma, alimpigia simu na kumuuliza kulikoni?
“Daah! Ilikuwa kero kweli, wanaume wazima wanaacha kazi zao na kuanza kunizomea huku wakiniambia kuwa ni dawa za Kichina. Lakini ukweli ni kuwa hii ni asili yangu na si Mchina,” alisema Amanda.
Hata hivyo msanii huyo amepewa angalizo na wadau kuwa kuna siku atakuja kufanywa kitu mbaya na wahuni kutokana na uvaaji wake wa nusu uchi awe mwangalifu sana.

No comments:

Post a Comment