TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, August 23, 2013

WAKATI KIPYENGA CHA LIGI KUU KIKIPULIZWA, SIMBA WAINGIA HOFU NA WAAMUZI, YANGA MWENDO MDUNDO WAAPA KUTANGAZA UBINGWA RAUNDI YA KWANZA TU. TFF WATOA RAI KWA MASHABIKI WA SOKA. DTV KURIPOTI LIVE LIGI HII!

 Wachezaji wa timu ya soka ya Simba ya Jijini Dar wakitoka nje ya uwanja msimu uliopita mwaka jana.
  Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na kati Dar Young Afrika wakipiga dua kabla ya mechi kwenye moja ya mechi zake msimu ulipita ambapo Yanga iliibuka kidede baada ya kuzigaragaza timu zote kongwe.

 Wachezaji wa timu Yanga wakishangilia moja ya magolo yake msimu uliopita ambapo wachezaji wa timu hiyo wameapa kufia uwanjani msimu huu kwa kutetea taji lao ambalo wanalishikilia wao.

Na Livingstone Mkoi
Wakati kipyenga kikipuzwa hapo kesho kwenye viwanja mbalimbali nchini kuashiria kuanza kwa msimu wa Ligi kuu ya Tanzania Bara Club ya Simba ya Jijini Dar imetoa angalizo kwa waamuzi wote wanaotarajia kuchezesha mechi za timu yao kuwa waangalifu. 

Akiongea na waandishi wahabari msemaji wa Club Ezekiel Kimwanga alisema kuwa wameamua kuweka tahadhari hiyo mapema kwa vile kumekuwa na mapungufu makubwa kwa waamuzi wa mchezo huo hivyo kwa vile mwaka huu mamilioni ya wa watanzania watashuhudia mechi hizo hivyo ni heri wakaepuka mapungufu hayo.
Aidha TFF imetoa rai kwa mashabiki wote kufika kwa wingi kwenye mechi za timu zote kwani Ligi ya mwaka huu itakuwa na upinzani mkali sana. Akiongea na waandishi wa habari msemaji wa shirika hilo Boniface Wambura alisema" Tunawaomba mashabiki wote wa mpira wajitokeze kwa wingi sana kwenye mecho zote kwani Ligi ya mwaka huu itakuwa na upinzani mkubwa sana kila kitu iko fiti kuikabiri timu pinzani" Alisema Wambura
Hata hivyo wa wachezaji wa timu ya Yanga wao wamesema kamwe hawatokuwa na huruma na timu yoyote itakayojitokeza mbele yao akiongea na Xdeejayz mmoja wa wachezaji wa timu Niyonzima alisema" Kaka kama mlivyoona kwenye mechi zetu za majaribio na ile ya Ngao ya hisani hatutakuwa na huruma na timu yoyote ile hapa ni kichapo tu tunahitaji kutangaza ubingwa raundi ya kwanza tu wembe uliotumika kunyoa msimu uliopita ndio utakaotumika mwaka huu" Alisema Niyonzima kwa njia ya simu
Aidha kituo chako bora cha DTV kupita Sport Live kinatarajia kuwalete taarifa zote za ligi kwa matukio ya picha na matukio.

No comments:

Post a Comment