Na Mwandishi Wetu
MAKAHABA nchini kenya sasa wanataka watambuliwe na wapewe ulinzi wanapokuwa kazini, ili na wao watoe kodi kwa serikali.
Kupitia chama chao, Africa Sex Workers’ Alliance (Aswa) wanawake hao
wanasema kwamba biashara yao ni sekta ambayo inatoa fursa nzuri kwa nchi
kujiendeleza kiuchumi.
“Tunataka watu watuangalie kama tunaoweza kusaidia kukuza uchumi huu na
wala si kuangalia kwamba tunaendeleza mmomonyoko wa maadili. Biashara
hii inaajiri mamia, kama si maelfu ya watu kote barani, akasema
mkurugenzi wa chama hicho, Bi Doughtie Ogutu.
Alisema chama cha Aswa kilianzishwa kwa madhumuni ya kutetea maslahi ya
wanachama ambao wamepitia mengi, yakiwemo kupigwa, kuuawa na hata
kulazimishwa kushiriki ngono na wanyama miongoni mwa mengine.
Ingawa wanaamua kuendelea na biashara hiyo, makahaba wanakiri kwamba
biashara hiyo ni hatari, hasa iwapo watapatana na wateja wabaya au hata
katika hospitali wanazokwenda kutibiwa.
Bi Ogutu anakumbuka miaka minane iliyopita pale mmoja wao alipopata
mteja Mzungu lakini akarejea akiwa maiti. Tena mwanzoni mwa mwaka huu,
wasichana wakakamatwa katika eneo la Pwani wakiwa na mwanamume mwengine
wa kigeni na kushtakiwa kwa kujihusisha na ngono isiyostahili - na mbwa.
“Hao wasichana hawakufanya hivyo eti kwa sababu walikuwa wakipenda.
Walilazimishwa. Nilienda Mombasa kufuatilia kesi hiyo. Ni kwa sababu
wanawake hawa hawalindwi na sheria. Wateja wao huwadanganya kuwa
watawalipa, lakini wanapofika nao kwenye nyumba zao ambapo hakuna hata
anayesikia ukipiga kelele, unafanya nini?” akauliza.
Kwa sasa, chama cha Aswa kinapanuka kutoka kuwepo katika mataifa kumi na
kinaelekea Magharibi na Afrika ya Kati. Lakini ushawishi wake hapa
Kenya umekumbwa na changamoto nyingi.
Maandamano
Mwaka jana mwezi Machi, tawi lake la Kenya Sex Workers Alliance (Keswa)
liliandaa maandamano kwenye barabara za jiji la Nairobi kutaka
wafanyakazi hao watambuliwe, ili wawe wakitozwa ushuru. Keswa walidai
kuwa na wanachama 40,000 ambao wanaweza kuchangia pakubwa katika uchumi
wa nchi hii.
Lakini kamati maalum ya Baraza la Jiji wakati huo, iliyoundwa na Meya
Goerge Aladwa kuangalia kama kuna faida ya kuruhusu makahaba kuendeleza
biashara yao, ilikataa mapendekezo ya wanawake hao.
Hata hivyo wachunguzi wa mambo wameomba Jeshi la Polisini nchini Tanzania kuwa macho na hali hiyo iliyotokea nchini Kenya kwani kuna uwezekano hata machangudoa wa hapa nchini wakaungana na wenzao wa huko kutaka matakwa hayo yatekelezwe.
No comments:
Post a Comment