HIZI
Inafaa tufahamu kuwa ili kuweza kujua ni siku zipi za
mwezi mwanamke anaweza kushika mimba (to conceive) inabidi tujua kwanza kipindi
ambacho mwili wa mwanamke uko tayari kushika mimba auOvulation Period. Ovulation
ni wakati ambao yai lililokua hutoka katika mirija ya ovari katika kizazi cha
mwanamke na katika wakati huu uwezo wako wa kushika mimba ni mkubwa. Kwa kawaida
mwanadamu huwa na mayai kadhaa katika ovari zake kwa wakati maalum wa mwenzi,
ambapo yai kubwa kuliko yote huondoka na kueleka katika tumbo la uzazi kupitia
mirija ya ovari. Ovulation haifuati mpangilio maalum kati ya ovari katika kila
mwezi na haijulikani ni ovari gani itatoa yai kila mwezi. Wakati yai linapotoka
huwa na uwezo wa kurutubishwa au kukutana na mbegu ya kiume na kuanza
kutengeneza mtoto kwa muda wa masaa 12 hadi 24, kabla halijapoteza uwezo wake.
Iwapo yai litafanikiwa kurutubishwa na mbegu ya kiume kwa wakati maalum na
kujikita katika fuko la uzazi basi matokeo yake ni mimba. Na iwapo
halitorutubisha yai hilo pamoja na kuta za kizazi huharibika na kutoka nje ya
mwili kama damu ya hedhi. Nimetangulia kueleza haya kama utangulizi kabla ya kuzieleza siku za kushika mimba kwani kuelewa suala hilo kutatusaida kujua umuhimu wa kujua idadi ya siku zetu za mzunguko wa mwezi (Menstrual Cycle) na umuhimu wake katika kushika mimba na hata katika magonjwa ya wanawake. Ili kuelewa vyema siku hizo inatubidi tujue kitu kinachoitwaKalenda ya Ovulation au kalenda ya kubeba mimba na pia tujua mzunguko wetu wa hedhi una siku ngapi. Mzunguko wa mwezi ni siku ya kwanza unayopata damu yako ya hedhi hadi siku kabla ya kupata tena hedhi nyingine.
|
Vipi kipindi cha Ovulation kinaainisha ziku za kubeba
mimba? Kipindi cha kubeba mimba huanza siku 4 hadi 5 kabla ya Ovulation, na humalizika masaa 24 hadi 48 baada ya hapo hii ni kwa sababu muda wa ovulation huweza kuchelewa au kuwahi kutokana na sababu mbalimbali. Pia kwa sababu mbegu ya kiume huwa na uhai kwa siku 4 hadi 5 na yai huweza kuishi kwa masaa 24 hadi 48 baada ya kuingia katika tumbo la uzazi. Hivyo kwa kujua siku hizo humsaidia mwanamke kufahamu kipindi chake cha Ovulation kimewadia na hivyo kuweza kukukutana na mumewe au mwenza wake wakati huo ili aweze kubeba mimba. Pia kujua kipindi hiki na masuala mengineyo kama hali ya joto la mwili ilivyo wakati wa Ovulation huweza kutumika kama njia ya kuzuia mimba. Yaani kutojamiiana katika kipindi hiki huweza kumzuia mtu asipate mimba. Kwa kuwa kipindi cha Ovulation hakina tarehe maalum na ni siku kadhaa, katika makala ijayo nitaendelea kuzungumzia baadhi ya alama za mwili zinazosaidia kutambua ni wakati gani Ovulation imewadia |
No comments:
Post a Comment