TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, May 20, 2013

MWALIMU WA CHEKECHEA ANASWA KWA UTAPELI,ANUSA KIFO KWA KIPIGO!

Tapeli hatari aliyefahamika kwa jina la Baba Kisiva akiwa ametapakaa damu baada ya kipigo toka kwa wananchi wenye jazba.

Tapeli akieleza kuwa yeye ni mwalimu wa shule za moja ya Chekechea Mkoani Arusha. Nakuomba asamehewe kwani alichokifanya ni njaa tu.



Wananchi wakimfunga kamba baada ya kumuokoa tapeli huyo aliendelee kupigwa na wananchi wenye hasira baada ya kutapeli laki nne kwenye duka la M PESA.





Wananchi wenye jazba wakiwa nje ya duka hiyo huku wakimuomba mwenye duka kumtoa nje tapeli huyo ili waendelee kumuadhibu.

  Baba Kisiva akiendelea kumuomba mwenye duka asimtoe nje wananchi wasije kumuua kwa kipigo
Begi alilokuwa nalo tapeli huyo likiwa na kisu pamoja na viwembe mbalimbali kwa ajili ya kudhuru watu.


Alitapeli  laki nne kwenye kibanda cha Tigo Pesa.Anusurik kifo kwa kipigo.
Na Livingstone Mkoi

Kijana mmoja ambae inadaiwa ni tapeli hatari Jijini Dar es Salaama aliyefahamika kwa jina la Baba Kisiva ambae anatokea Muarusha wiki iliyopita alinusurik kifo baada ya kutapeli shilingi laki nne dukani kwa mangi.

Tukio hilo la aina yake lilitokea maeneo ya Kinondoni Mkwajuni karibu na baa ya Maridadi “ Makao Makuu” na kushuhudiwa na mamia ya wananchi huku akiponea chupu chupu kuchomwa moto na wananchi wenye jazba kubwa.

Akiongea na Xdeejayz Wakala wa huduma za kurusha pesa kulikofanyika tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Gradstone Fanuel alianza kumueleza mwandishi wetu kuwa kijana huyo alifika dukani kwake na kumtaka amrushie shilingi laki nne kwenye simu yake haraka.

Hata hivyo kutokana na kutomtilia shaka mteja huyo wakala huyo alifanya kama mteja wake alivyohitaji.Baada ya kufanikisha kutuma pesa na meseji kuonesha kuwa pesa ilitumwa kwenye simu namba 0755-689171 na kuonesha jina la mtu aliyepokea pesa hiyo kuwa ni Dokta John Katoko.

Aidha baada ya kumuonesha mteja wake hiyo iliyosomeka kuwa “Q56EI038 imetumwa kwa DOKTER JOHN tarehe 9/5/13 saa 5:44 PM Salio lako….. Tsh……” Ambapo mteja wake alianza kuingiza mkono mfukoni ili kutoa pesa kiasi hicho cha shilingi laki nne.

Hata hivyo muda ulizidi kwenda huku hakuna matumaini ya kutoa huyo pesa huku akionekana kupiga mahesabu ya kumkimbia wakala huyo ambae ni maarufu maeneo hayo ambapo haraka aligundua kuwa mteja wake huyo alikuwa tapeli ndipo wananchi walianza kumtia adabu.

Aidha katika hali isiyotarajia dakika moja tu baadae iuligundulika pesa hiyo ilikuwa imeshatolewa kwenye simu namba  Dodwin Listen Godwin hasa baada ya kuulizia makao makuu ya mtandao husika.Baada ya kibano kikali toka kwa wananchi huku wakimtaka kijana huyo kujieleza kuwa anatokea watu ndipo alisema kuwa anatokea Mwananyamala lakini ni mwenyeji wa Arusha na kule yeye ni mwalimu wa shule moja ya Academi ambayo alishindwa kutaja jina.

Hata hivyo kijan huyo aliwashukuru madalali wenye ofisi karibu na dula la wakala huyo ambao walimsaidia kumuokoa na kumuingiza dukani kwa aliyetapeli hadi polisi walipofika kumuchukuwa na kumpeleka kituo cha Oysterbay kasha kumfungulia jarada OB/RB/8212/ UWIZI WA PESA KUTUMIA MTANDAO.

Imeelezwa kuwa vijana hao wako sita hivyo wakati wa kwenda kutapeli hujipanga wawili wawili kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo la utapeli hivyo inadaiwa wameshawaliza watu wengi sana hivyo wakazi wa Jijini wameliomba jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali wale wote wanaokuwa wanakamatwa kwa makosa hayo ili kukomesha matukio hayo.

No comments:

Post a Comment