TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Sunday, May 19, 2013

GOLI LA DIDIER KAVUMBAGU KWA SIMBA NUSRA LIMTOE ROHO JB,AONDOKA MAPEMA UWANJANI!


 Msanii JB kulia akiwa na Masanja Makandamizaji

 Msanii JB kulia

 Msanii JB kulia ambae ni shabiki mkubwa wa timu ya soka ya Simba, Huku akiwa amevalia tisheti ya timu hiyo.

Na Livingstone Mkoi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida goli la dakika ya nne lililofungwa na mchezaji Didier Kavumbagu dhidi ya Simba nusra limtoe roho msanii nyota wa filamu za Kibongo Jb ambae ni shabiki wa Simba.

Mapapalazi wetu waliokuwa wamesambaa kila viunga vya uwanja huo walimshuhudia JB ambae aliingia uwanjani hapa majira ya saa tisa na robo za jioni akiwa ameongozana na Shamsa Ford pamoja na wasanii wengine.

Aidha baada ya kufika uwanjani hapo kama kawaida akiwa amevalia uzi mwekundi pamoja na kitu chekundi alikwenda moja kwa moja hadi jukwaa la Simba na kukaa.

JB ambae awali alionekana kuwa mchangamfu na mwenye matuamaini ya ushindi kwa timu yake ambapo katika hali isiyotarajia mara baada ya mpira kuanza ndani dakika nne mshambuliaji hatari wa Yanga DIdier Kavumbagu aliiandikia tumu yake goli la kwanza baada ya  kupigwa kona.

Msanii huyo alijikuta anang'onyea kabisa na kupoteza uchangamfu,Hata hivyo hali ilikuwa mbaya baada Yanga kuongeza goli la pili kupitia kwa mchezaji wale Hamis Kiiza Jb alipoteza matumaini kabisa. 

No comments:

Post a Comment