TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, April 30, 2013

MWANAMUZIKI DIAMOND ATABIRIWA MWISHO WAKE UMEFIKA!

Mwanamuziki Diamond akiwa kwenye picha ya pozi.

Na Livingstone Mkoi aliyekuwa Arusha

Mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki nyota wa nchini Diamond wameonesha wasi wasi wao kuwa huenda siku za kutamba mwanamuziki huyo zinahesabika kutokana na wimbo wake alioutoa hivi karibuni kuwa mbovu ile mbaya.

Wakiongea Xdeejayz mashabiki hao wanaoishi Arusha mjini walisema kuwa" Hakika acheni usemi wa wahenga utimie kuwa Ngoma ikivuma sana mwishowe lazima ipasuke huu wimbo wa Mapenzi Basi wa Diamond hamana kitu kabisa awali tulishindwa kuamini kama ni yeye kaiba au alikuwa ameshirikishwa" Alisema dada mmoja aliyejitaja kwa jina la Grace

Aidha mashabiki hao waliendelea kuweka wazi hisia zao kna kusema Diamond kwa sasa anatakiwa kujipanga kwa ajili ya kufanya mambo mengine kwani dalili hizo ni mbaya kwa wanamuziki hasa wanapokuwa maarufu kama yeye kwani wameshuhudia mwengi tu mfano kama Mr Nice, Dudubaya, Juma Nature nk ambao enzi zao walikuwa kama Diamond huku kila nyimbo wanazotoa zilikuwa juu lakini baadae walianza kutoa nyimbo mbaya mfano wa hii ya Mapenzi Basi.


No comments:

Post a Comment