Mkusanyiko wa watu kama huu ndani ya kituo cha mabasi Ubungo umedaiwa kuongeza maambukizi hatari ya ugonjwa wa ukimwi.
Eneo la kituo cha mabasi Ubungo kama kinavyoonekana.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh John Mnyika.
Na Livingstone Mkoi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushtua kumeibuka taarifa za kutisha juu ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa ukimwi yanayoendelea katika kituo cha mabasi cha Ubungo kwa sasa.
Xdeejayz ifunga safari hadi kutuoni hapo baada ya kutonywa na baadhi ya wahudumu wa kituo hicho na kusikitishwa na mienendo ya maisha ya vijana yanavyokuwa hatarini.
Wakiongea na mwandishi wetu kituoni hapo kwenye mahojiano maalum wahudumu hao walisema kuwa ki ukweli hali ya maisha ya vijana kwenye kituo hicho ni mbaya sana kwani kwani kila kukicha kunaibuka maambukizi mapya.
Mmmoja wa akina dada ambae ni muhudumu wa kituo hicho alianza kusema" Kaka hali ni mbaya kwa kweli hapa Ubungo kuna nuka ngono ukimwi unatekekeza vijana hasa hawa maajenti wengi wameathirika sana hivyo kuna mzunguko mkubwa sana wa maradhi hayo hapa, na inatakiwa juhudi za haraka kuchukulwa ili kuwanusuru vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa" Alisema Dada huyo ambae aliomba hifadhi ya jina lake
Hata hivyo dada huyo aliendelea kusema" Mara nyingi maajenti wengi wanaponzwa na tamaa kwani kuna wafanyabiashara wa kila aina hivyo wakija kama kuchukuwa tiketi kisha humuachia hela ya soda kama laki hapo ndipo hunaswa kwani hufikiri kuwa kama soda tu kampa laki je akitembea nae si atampa mamilioni ya fedha" Kilisema chanzo hicho
Baadhi ya watu katika soko hilo wametoa uwito kwa mbunge Jimbo hilo ndugu John Mnyika kufanya jitihada za kuwaelimisha vijana hao la sivyo miaka kumi mbili hali itakuwa mbaya kwani kwa sasa kinachofanyika ni kuambukizana makusudi tu wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment