TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, January 29, 2013

BLOG YA XDEEJAYZ YATIKISA NCHINI AFRIKA KUSINI,MTANGAZI WA AFRIKA MAGIC SWAHILI KUINGIA NAYO UBIYA WA MATANGAZO!

 Mtangazaji ambae ni mtanzania anayetangaza Afrika Magic Swahili, nchini Afika Kusini  Fortunatus Kasomfi akiwa picha ya pamoja na mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu.

Fortunatus Kasomfi

Na Livingstone Mkoi
Mtangazaji nyota wa Radio Afrika iliyopo nchini Afika Kusini ambae nia ni ripota wa Afrika Magic Swahili Fortunatus Kasomfi amesema anamikakati ya kuingia mkataba  wa kufanyakazi na blog hii inayoongoza kwa sasa kuwa na wasomaji kwa vile imekuwa blog pekee inakubarika nchini Afrika Kusini.

Fortunatus ambae pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Forjoys Art Production Inc yenye makazi yake Johannesburg  aliendelea kusema kuwa licha ya nchi ya tanzania kuwa na utitili wa blogs lakini watanzania wengi waishio nchini Afrika Kusini hupenda sana kutembelea blog ya xdeejayz kutokana na kuwa na habari za uhakika pamoja na picha matukio ya kusisimua.
Aidha mtangazaji huyo ambae kwa sasa yupo nchini Ujerumani kikazi na mwisho wa mwezi ujao atarejea nchini Afrika Kusini kisha kurudi nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa blog hii ambao ni kampuni ya  Entertainment Masters Ltd
Hata hivyo Fortunatus alimaliza kusema kuwa kutokana na kampuni yake kushughulika na mambo ya sanaa hivyo itakuwa njia nzuri kwa kufanya kazi pamoja na xdeejayz ambayo kimsingi imekaa kiburudani zaidi pamoja na habari.

No comments:

Post a Comment