TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, January 29, 2013

MWANAMUZIKI ALEX WA MACHEJO ANUSURIKA KUULIWA,WANANCHI WENYE HASIRA WAMJERUHI VIBAYA !

 Mwanamuzi wa bongo flava Alex Machejo akiwa na baadhi ya wasanii wa komedi


 Alex Machejo akiwa nyumbani kwa bibi yake mwananyama Jijini Dar akijiuguza pichani kama anavyoonekana siku alipotembelewa na mwandishi wa Xdeejayz


Na Livingstone Mkoi

Katika hali ya isiyokuwa ya kawaida na kusikitisha mwanamuziki nyota wa bongo flava Alex wa Machejo hivi karibuni alinusurika kuuliwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutupiwa mdudu.

Habari za uhakika toka kwa mwananmuziki huyo zilisema kuwa ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu akiwa nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni Moscow Jijini Dar es Salaam usiku ghafla alisikia kizunguzungu pamoja na kiza nene machoni mwake kisha akadondoka.

Hata hivyo hali hiyo aliichukuliwa kama ni kawaida tu.Lakini cha ajabu hali hiyo haikumuacha hadi siku iliyofuata ambapo sasa mambo yalibadilika ambapo akaanza kupiga kelele kama mtu mwenye kichaa.

Mwanamuziki huyo aliendelea kusema kuwa alianza kukimbia ovyo  huku wananchi wakimuungia kwa kupiga kelele za mwizi pamoja na kuanza kumpiga kwa mawe na nondo kichwani.

Lakini hata hivyo baadhi ya watu wanaomjuwa mwanamuziki huyo walifanikiwa kumuokoa mikononi mwa wananchi wenye jazba kali kwa kumtetea kuwa hakuwa mwizi bali anaumwa.

Alex aliiambia xdeejayz kuwa hafahamu ni kwa nini watu wabaya waliamua kumfanyia hivyo kwani uchunguzi umebaini kuwa alitupiwa mdudu mbaya na bila nguvu za mungu ilibidi afe kwa kipigo cha wananchi au awe mwendawazimu.

Timu ya waandishi wa xdeejayz inampa pole mwanamuziki huyo na mungu amjalie arudi kwenye hali ya kawaida ili kuweza kuendelea na majukumu yake ya sanaa kwa ajili ya ujenzi wa taifa.



No comments:

Post a Comment