TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, December 3, 2012

AIBU KUBWA! BONGO MUVI WADAIWA KUIBA KATONI ZA SODA NA MAJI YA WAFIWA KWENYE MSIBA WA SHARO MILIONEA!



MMOJA WA VIONGOZI WA KUNDI LA BONGO MUVI JB

Ni zile ziliotolewa na Bakhresa kama msaada kwa wafiwa.
Polisi,Wafiwa washikwa na butwa. JB agoma kuongea na Xdeejay.


Na Mwandishi Wetu Tanga.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushangaza kundi la Bongo muvi limekumbwa na kashfa kubwa na ya kufunga 2012 baada yaa kudaiwa kuimba katoni za Maji,Juisi na Soda aina ya Azam Cola kisha kukimbia nazo ndani ya basi na kuacha ndugu wa marehemu wakiwa na mshangao mkubwa.

Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na kila mtu pamoja na baadhi ya Askari Polisi ambao walikuwa wamekusanyika nyumbani kwaa marehemu kwa ajili ya kutoa msaada kwenye msiba huo ulitokea mwanzoni mwa wiki hii Mkoani hapa.

Habari za uhakika toka eneo la tukio zilisema bongo muvi walianza kuonesha madudu yao kabla hata ya kuzika mwili wa marehemu kwani walipoingia tu kwenye viunga vya nyumba ya msiba walianza kujiliza kwa kuigiza huku wengine wakijizimilisha hali iliyoleta tafsiri tofauti kwa watu waliohudhuria.
Hata hivyo ukiaacha vituko hivyo pia kunaa matukio mengine yaliyojitokea ni pamoja na kushindwa kukalia mikeka iliyokuwa imekaliwa na watu waliokuwepo tangu siku ya awali lakini wapofika wasanii hao walilazimika kuomba kukalia viti ili wasichafuke.

Pia hali hiyo iliwakera watu wengi lakini walishindwa kusema kwa vile kila mtu alikuwa bize na mambo ya msiba.Hata hivyo baada ya kumaliza kusema Bongo muvi ambao walikuja mkoani hapa na mabasi mawili ya Simba Mtoto walianza kukimbilia kwenye magari hayo bila hata kuingia ndani tena kuwaaga vizuri ndugu na wafiwa.

Hata hivyo wakati wanaingia kwenye magari hayo wasanii nyota Mtunisi pamoja na Eliya Mjata waliwachukuwa vijana kadhaa na kuingia nao ndani kisha kuanza kusombelea kantoni za Juisi,Azam Cola pamoja na za Maji hadi kubaki machache tu.

Baada ya kumaliza kusombelea maji hayo waliwasha gari na kuondoka na kurejea Dar huku kila mwanachi akishangaa kwa tukio hilo,Kufuatia taarifa hizo Xdeejayz ilimtafuta mmoja wa viongozi wa kundi hilo JB kupitia simu yake ya mkononi iliyopigwa saa 00:01:24 Pm Jumapili ambapo aligeuka mbogo kwa mwandishi wetu.

JB alishindwa kuonesha ushirikiano wowote zaidi ya kufoka na kujibu kimkato” Sema nani?” JB alimuuliza mwandishi wetu na baada ya kushushiwa tuhuma za wasanii wake alijibu” Hivi nyie huwa hata mnasali kweli au kupumnzika na familia zenu,Mimi nipo na Mke wangu nimepumnzika leo Jumapili ebu naomba mniache jamani nitafuieni siku ya kazi” Hayo ndiyo yalikuwa majibu ya JB.





No comments:

Post a Comment