TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, November 6, 2012

MASELE WA KOMEDI ASAKWA KWA TUHUMA ZA WIZI!

Faili lake ni SO/IR/4417/2012 "WIZI WA SIMU" 
SONGEA-RUVUMA
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma wilaya ya Songea linamtafuta kwa udi na uvumba muigizajia maarufu wa Komedi nchini Masele kwa tuhuma za uwizi wa simu na Galaxy.
Habari za uhakika toka mtu aliyeibiwa zinasema kuwa Masele aliiba simu hizo kisha kukimbia na kuacha vilio tele.

Akiongea na mwandishi wetu dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Amina Vicent alisema kuwa Masele alikuwa Songea kwa ajili ya shoo akiwa ameandamana na wanamuziki wengine kama Ney wa Mitego,Masai mbofumbofu na walikuwa wanaimba kwenye tamasha lililoitwa Cross Road.
 Kesho yake walikuwa wanaondoka kurudi Dar Lakini kwa bahati mbaya Masele akaachwa na gari ndipo jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Papa alipomkaribisha nyumbani kwake lakini asubuhi kulipoamka hakumkuta huku siku zake mbili aina ya blackbery hazikuwepo huku pia Galaxy ya msichana Amaina nae ilikuwa imeshachukuliwa.
Hata hivyo baada ya tukio hilo watu hao waliamua kwenda kumfungulia taarifa Polisi msanii huyo na kupewa namba ya utambulisho SO/IR/4417/2012 "WIZI WA SIMU" Na hadi sasa bado anatafutwa.
Kona hii ilimptafuta Masele kupita simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo ambapo msanii huyo alipatikana na kujibu" Huyo dada ana matatizo anataka kujipatia umaarufu kupitia mimi kwanza hivyo mimi nitamfunga nini wanasheria wangu ambao nao hawapendi kusikia kashfa za uwongo kama hizo" Alisema Masele na kukata simu

No comments:

Post a Comment