TANGAZO MAALUM
.
TANGAZA NA SISI
Friday, March 28, 2014
ANGALIA PICHA ZA OMMY DIMPOZ ANAVYOENDELEA KUKIMBIZA HUKO UMANGANI..!

Siku kadhaa baada ya kutua Tanzania akitokea Marekani na Uingereza alikokwenda kufanya show pia, Ommy Dimpoz amepata dili jingine zuri kwa kualikwa kuimba na band yake aliyotoka nayo bongo katika party ya kampuni ya mafuta huko Muscat Oman.


Kwa siku kadhaa Ommy ambae ni miongoni mwa vijana wachache wa bongofleva wanaosifika kwa kujituma na kuwa serious na kazi, alionekana akifanya mazoezi na band yake ambayo ndio atahusika nayo mwanzo mwisho kwenye stage siku ya show Ijumaa March 28 2014
CREDIT: XDEEJAYZ
NJAA MBAYA JAMANI ANGALIENI SIMBA ALIVYOMCHENJIA MAMBA KISA MZOGA WA KIBOKO UTADHANI ANAWEZA KUUMALIZA WOTE..!











Ni
jambo la nadra sana kuona wanyama wanaosifika kwa kuwala wenzao mbugani
kuonekana wakipambana, katika picha hizi zilizopigwa na mtaalam wa
masuala ya teknolojia kutoka San Francisco nchini Marekani, Richard Chew
aliyekuwa kwenye mapumziko na mke wake kwenye mbuga ya Maasai Mara
iliyopo Kenya aliweza kunasa tukio la mamba akipambana na Simba mwenye
njaa wakigombea mzoga wa kiboko aliyekufa, nisikuchosh.
CREDIT:XDEEJAYZ TANZANIA
UKUHADI WAMTOKEA PUANI PATCHO MWAMBA, WOLPER NA PEDESHEE LA KIKONGO WAITEKA NCHI KWA MAHABA..!
Mambo hadharani! Kigogo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayewagombanisha mastaa wawili Bongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid ni huyu hapa.
Anaitwa Rajab Mwami Shamweshi.
Habari zilizolifikia Ijumaa zilidai kwamba
baada ya mtafaruku wa mastaa hao kuripotiwa na gazeti mama la hili,
Uwazi la Jumanne iliyopita, jamaa huyo aliibuka na kuanza kulalamika kwa
watu wake wa karibu kuwa anachafuliwa mitandaoni kwa sababu ya mastaa
hao.
PATCHOU MWAMBA NDANIIlidaiwa kuwa Mwami alichukizwa na ishu hiyo kwani ilimhusisha mwanamuziki wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia ni mwigizaji, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ kuwa ndiye humkuwadia kwa mastaa.
TUANZE NA PATCHOU
Kabla ya kumpata Mwami mwenyewe, Ijumaa lilizungumza na Patchou uso kwa uso amba alifunguka anachokijua juu ya sakata la Wolper na Husna kumgombea mwanaume huyo.
Alisema: “Mimi nashangaa kuona nachafuliwa mitandaoni lakini ukweli anayefanya hivyo ni Husna.
“Huyo Husna ni kweli aliwahi kutoka na Mwami lakini baadaye alimdharau Mwami kwa sababu alimuona hana pesa.
“Baada ya kuona pesa zimemtembelea Mwami akataka kurudi ndipo akakuta jamaa ameshajiweka kwa Wolper. Hapo ndipo Husna akaanza kuchanganyikiwa.” Patchou aliendelea kuweka wazi kwamba yeye na Mwami ni mtu na rafiki yake na pia ni ‘mapatna’ kwenye biashara.
Alisema amekuwa akikutana naye mara kwa mara Nairobi, Kenya na ndiye aliyemleta Bongo kwa ajili ya kuanzisha kampuni ya michezo ambapo alifikia hotelini.
KUWADI?
Alitiririka kwamba hajawahi kumkuwadia mwanamke lakini anachojua Mwami ni anajuana vizuri na
Wolper kwani alimtambulisha walipokutana Nairobi hivi karibuni ndipo akaujua uhusiano wao.
Patchou: “Nilishangaa kwa sababu baada ya Mwami kutua tu Bongo, wasichana wa mjini walipojua
ndipo wakaanza kumsaka hadi chumba alichofikia hotelini.“Wengine walidiriki hata kumtumia picha za utupu ili kuwa naye kimapenzi baada ya kupata namba yake.”
Patchou alisisitiza kuwa yeye si kuwadi kama wanavyomtangaza kwani hata huyo Wolper alishtukia amekutana naye Nairobi wakiwa na Mwami kwani kabla ya hapo alikuwa hajuichochote.
Baada ya kumaliza kutoa utetezi wake, aliombwa kumpigia simu Mwami na kumuweka loud speaker
(sauti ya juu) ambapo alimweleza Mwami kila kitu ndipo akakubali kuzungumza na wanahabari wetu akiwa London, Uingereza.
KIGOGO AFUNGUKA
Akizungumzia sakata hilo, Mwami ambaye anadaiwa kuwa na ‘mihela’ hivyo kujitwalia taito ya ukigogo alisema kuwa anamfahamu Husna kama mtu wa kawaida ambaye aliwahi kufahamiana naye.
KUHUSU WOLPERKwa upande wa Wolper alisema kuwa anamfahamu kwa kumsikia na kumuona lakini si kimapenzi kama wanavyomchafulia jina.
“Nilipokuja Tanzania kwa mara ya kwanza nilifikia hotelini…(anaitaja), kama wanavyodai hata chumba ndicho chenyewe lakini sikuja kwa ajili ya starehe za kimapenzi na wanawake, nilikuja kwa biashara zangu, nashangaa kuona nawekwa mitandaoni hovyo na anayeniweka namfahamu.
“Naomba nisizungumze sana, niishie hapo nikirudi Tanzania nitaongea nanyi kwa uwazi kabisa,” alisema Mwami.
Wolper na Husna ambao waliwahi kuwa mashosti walianza manenomaneno hivi karibuni ambapo awali haikujulikana chanzo hadi pale Husna alipoamua kulifungukia hilo la mwanaume.
Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka Wolper kupitia simu yake ya mkononi, alipopatikana alisema angefika ofisini kwetu kutoa ufafanuzi lakini mpaka gazeti linakwenda mtamboni alikuwa hajafika na alipotumiwa sms ya kuulizwa kama angefika au la hakujibu.
WAISLAM KUMTENGA DIAMOND KISA UPUUZI HUU ANGALIA HAPA ALICHOKIFANYA KINASHANGAZA..!
KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewachefua waumini wenzake wa Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.
Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo kulifanyika Maulidi ya kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.
Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini kadiri walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza kuharibika.
“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya
Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai
chanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.
Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza
staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.
“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza
Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.
Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho
likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.
Thursday, March 27, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)













