TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, April 2, 2016

HATARI KUBWA: WANANCHI WALIOKUNYWA MAZIWA YA FISI WAKIDHANI YA NG'OMBE WAINGIWA HOFU MKOANI TABORA, DOKTA KAMDEGE KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI. MASKANIBONGOTZ INAKUPA MKASA MZIMA...!


 HAPA MKUU WA KITENGO CHA HABARI  ZA UCHUNGUZI TOKA E-FM RADIO KULIA BW LIVINGSTONE MKOI AKIONESHWA MLIMA AMBAO NG'OMBE HAO WALIOGEUKA FISI WALIPOKIMBILIA BAADA YA KUGEUKA KUWA FISI MKOANI TABORA NA ANAETOA MAELEKEZO HAYO NI KIJANA ALIYEKUWA AKIWACHUNGA NG'OMBE  HAO WA KICHAWI.
HAWA NI BAADHI YA NG'OMBE HALALI WALIOBAKI BAADA YA WENGINE KUGEUKA KUWA FISI.



 MAHARA HAPA NI SEHEMU YA ZIZI LA NG'OMBE WALIOKIMBILIA MSITUNI BAADA YA KUGEUKA KUWA FISI KWENYE KIJIJI CHA UKANGA WILAYA SIKONGE MKOANI TABORA
 MCHUNGAJI WA NG'OMBE HAO ALIYEJITAMBULISHA KWA JINA LA MUSA MAJIHA AKIHOJIWA NA MWANDISHI WETU BW LIVINGSTONE MKOI HAYUPO PICHANI
 DOKTA KAMDEGE MTAALAMU WA MITI SHAMBA AKIWA NJE YA OFISI YAKE MKOANI TABORA TAYARI KUELEKEA KWENYE KIJIJI KISANGA NJE KIDOGO YA WILAYA YA SIKONGE KWA AJIRI YA MPAMBANO NA KUWATOKOMEZA FISI HAO.
HII NDIYO OFISI YA DOKTA KAMDEGE KAMA INAVYOONEKANA.

Na Waandishi wa maskanibongotz- Tabora
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni hivi ndivyo tunavyoweza kusema kufuatia mzee mmoja Mkoani Tabora amekuwa akiwanywesha watu maziwa ya Fisi zaidi ya miaka 25 sasa, huku watu wengi wakidhani ni Ng'ombe huku maziwa hayo yakiwa matamu kupita kiasi.
Tukio hilo la kushtua lililoripotiwa na kituo cha E-fm Radio hivi karibuni, ambapo katika habari hiyo wakazi wa Kijiji cha Ukanga kilichopo Wilaya ya Sikonge  wakimlalamikia mzee huyo wa kisukuma kwa tukio alilowafanyia.
Habari zaidi zilieleza kuwa mtaalamu wa miti shamba Dokta Kamdege ndiye aliyegundua kuwa maziwa hayo si halali baada ya wananchi eneo hilo kumuita mtaalamu huyo kwa ajiri ya kuwasaidia mambo mengine lakini akiwa huko aligundua tatizo la maziwa hayo ya fisi.
Mzee huyo alikuwa na ng'ombe zaidi ya mia na hamsini huku ng'ombe halali wakiwa 50 tu na mia wakiwa ni fisi pamoja na watoto wao ambao kwa macho ya kwaida walikuwa wanaonekana ni ndama wa ng'ombe.
Hata hivyo  baada ya mganga huyo kugundua hali hiyo wananchi waliitisha mkutano mkubwa na kumuomba mganga huyo awasaidie kuhusu tatizo hilo, ndipo alipokwenda kwenye zizi la mganga huyo lakini walikutana na mtihani mkubwa kwani mzee huyo alikuwa ametega umeme kwenye zizi hilo na ukamnasa mmoja wa wasaidizi wa Dokta Kamdege hadi kupoteza fahamu kwa muda kabla hajapatiwa huduma ya kwanza.
Kwa mujibu wa Dokta Kamdege alisema umeme huo ulikuwa wa kichawi kwani katika eneo hilo la polisi bado hakuna maendeleo ya umeme, hivyo ndipo walipomwaga dawa zake kisha ng'ombe hao walianza kugeuka fisi kisha kukimbilia polini na kubaki wale ng'ombe hamsanini halali.
Kutokana na tukio hilo  kuna uwezekana Dokata Kamdege akahojiwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo ili kujua kama maziwa waliyokunywa wananchi hao yana madhara ama laa, kwani Serikali haiamni uchawi lakini yeye ndiye mtu aliyegundua hayo.
Akiongeo na matndao huu kwa simu namba 0788-844490 Kamdege alisama " Ndugu mwandishi haya ni mambo ya kishirikina hata mimi imenihudhunisha sana kuona wananchi wakinyweshwa maziwa ya fisi hali ambayo sisi tuliojaliwa na Mungu kuwa na vitu vyema kichwani ni lazima tuwasaidie na haieleweki kama watakuja kudhurika ama laa" Alisema Kamdege
Na pia alitoa uwito kwa watanzania mahali popote kama kuna mambo ya ajabu wanafanyiwa au wanahisi kama maisha yao hayaendi vizuri, mipango wanayoipanga hatimii basi wawahi kumjurisha ili awasaidie hayo yote yanafanywa kutumia miti shamba tu wala sio uchawi au ndumba, pia hata kukwamba kwa biashara.  maradhi yalishindikana, kushindwa kupata kazi licha ya kwamba watu wengi wamesoma na kuwa na ujuzi lakini wabaya wameziba ridhiki basi hayo yote yanafunguliwa kwa dawa maalum za miti shamba.


Hata hivyo wananchi hao kwa nyakati tofauti walisema kuwa hadi sasa wana hofu kutokana na kunywa maziwa hayo kwa kipindi kirefu hivyo wasi wasi wao huenda yakawaletea madhara siku za usoni
Credit: Maskanibongotz

Friday, April 1, 2016

HIVI NDIVYO UKIMWI UNAVYOWAMALIZA WAFANYAKAZI KITUO CHA MABASI UBUNGO,WAFANYAKAZI WA KIKE WAONGOZA KWA MAAMBUKIZI, , ROBO TATU YA WASICHANA MAAJENTI NI WAATHIRIKA, MUHANGA MWENZAO ATOA SIRI NZITO PIA WAPO WANAOTEMBEA NA MABOSI ZAO KWA SIRI...!



Na Waandishi wa Maskanibongotz/ Sadiktv
Katika hali ya kushtua mtandao huu wa Maskanibongotz umepokea taarifa za kushtua juu ya kuwepo kwa hali ya hatari kwenye Kituo cha Mabasi Ubungo kufuati kuwepo kwa maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi huku wahanga wakubwa wakiwa ni baahi ya wanawake wanaojihusisha na  ukataji tiketi maaraufu kama mawakala na maajenti.
Kikosi cha waandishi wetu wa habari za uchunguzi baada ya kupata taarifa hizo waliamua kufunga safari hadi ndani ya kituo hicho cha  kikubwa na chenye umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na nje kutokana na kutoa na kupokea mabasi yanayokwenda nchi mbalimbali Afrika.
Mara baada ya waandishi wetu kutua kituoni hapo walikutana na  mtoa habari wetu ambae ni Dada mwenye maambukizi ya Ukimwi jina linahifadhiwa kama anavyoonekana pichani ambapo aliwakalisha waandishi wetu kitako na kuwaeleza ishu nzima jinsi ukimwi ulivyotapakaa huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake huku ikidaiwa karibia robo tatu ya wasichana wanaonekana hapo ni waathirika.
Dada huyo ambae ni mwenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro alisema alianza kazi ya ukatishani tiketi tangu mwaka 2006 hadi kampuni anayofanyia kazi mabasi yake yanakwenda Mikoa ya Arusha na Moshi na hata maradhi ameyapata hapo hapo akiwa kazini.
Akiongea kwa majonzi makubwa Dada huyo ambae ana watoto waweili ambao bahati nzuri aliwazaa kabla hajakutwa na janga hilo alisema" Ndugu zangu hali ya hapa ni mbaya ukimiwi umesambaa kama upepo, msione mabinti wamenona hivyo na kujazia hivi wote hapa tuna VVU mimi nisema ukweli tu hata nikificha haisaidii, mfano chumba no****** hao wadada wote mabonge wameshaathirika" Alisema  Dada huyo kwa muonekano wa macho kamwe huwezi amini kama ni mgonjwa
Msichana huyo aliendelea kusema " Sababu kubwa inayotuponza ni tamaa kwani kama mnavyojua hapa wanakuja watu wa kila aina tena wenye madini ya kutosha hivyo ni rahisi mtu kuingia kwenye mtego, lakini wapo wasichana wengine wanatembea na mabosi zao ambao ni wamiliki wa mabasi na wamewafanya nyumba ndogo zao huku majumbani kwao wakiwa na wake zao halali hivyo hali hiyo inapelekea maambukizi kusambaa kwenye familia zao" Alisema
Hata hivyo mdada huyo alisema kuwa kikubwa tamaa tu ndiyo inawaponza kwani kama pesa wana pata sana kwenye kazi zao halali za uajenti huku wengi wakishiri michezo ila tamaa za mwili kuwa mpenzi zaidi ya mmoja ndiyo pia inachangia, na pia kutokana na urembo wa maajenti hao huku wengi wao wakiwa mshalaah pia abiria wengi wanapokuja kukata tiketi hunasa kiulaini.
Dada huyo alimalizia kutoa ushauri wake " Kaka tunaomba kupitia habari hii vyombo vinavyohusika kuelimisha kufika hapa Ubungo terminal kwa ajiri ya kutoa elimu la sivyo miaka 10 mbele watu wengi tutakuwa tumeondoka duniani, Mimi najua ni wa kuondoka leo kesho licha ya kwamba nimeanza dozi lakini najua nitakufa hivi karibuni sitokuwa na maisha marefu" Alisea dada huyo kwa masikitizo
Hata hivyo mtandao huu pia ulibata bahati ya kuongea na mpiga debe mmoja ambae nae pia aliomba hifadhi ya jina lake lakini alikuwa na haya ya kusema" Jamani ndugu waandishi Ubungo inatisha kwa maambukizi yani mfano ikitokea labda kila chuamba cha ofisi watu wakapimwa majibu mtakayoyapata hapa Tanzania itatikisika, na sasa kwa vile tupo wanaume na wanawake hivyo wengi wanatembea pamoja kwa kushiriki tendo la ndoa huku pembeni wakiwa na wapenzi wengine hali inayoongeza maambukizi" Alisema
Mtandao huu unashauri mamlaka zinazohusika na kuelimisha kuhusu gonjwa hili kufanya ziara za mara kwa mara kituoni na kutoa elimu kwani la sivyo tuapoteza nguvu kazi kubwa ya Taifa.
Source Maskanibongotz

Magazeti Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 1 2016 kwenye, Udaku, hardnews na michezo


20160401_050415-1
20160401_050445-1
20160401_050458-1
20160401_050517-1
20160401_050526-1
20160401_050544-1
20160401_050553-1
20160401_050630-1
20160401_050644-1
20160401_050655-1
20160401_050713-1
20160401_050741-1
20160401_050800-1
20160401_050810-1
20160401_050824-1
20160401_050838-1
20160401_050856-1
20160401_050908-1
20160401_050928-1
20160401_050936-1
20160401_050957-1
20160401_051021-1
20160401_051037-1
20160401_051054-1
20160401_051115-1
20160401_051137-1
20160401_051250-1
20160401_051315-1
20160401_051415-1
20160401_051437-1
Kama ilikupita Video ya magoli ya Yanga Vs Ndanda FC FA CUP March 31 2016, Full Time 2-1