Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi mkali kituo cha Polisi CCM Mwinyijuma Mwananyamala.
Kushoto ni Afande Makomeo ambae alipongezwa na wananchi kwa kuwakamata watuhumiwa hao hatari
Watuhumiwa hao wakishangaa mwanga wa kamera za waandishi wa mtandao huu wa maskanibongtz, watuhumiwa hao walifanyahamika kwa majina ya Seif Ramadhani pamoja na Ahameg Mwalimu ambapo huyo mweupe alikuwa amewatishia askari hao kuwa yeye ni Mwanasheria na ahata alivyoombwa aoneshe kitambulisho hakuwa nacho.
POLISI KINONDONI WAKAMATA WAFANYABISHARA SUGU WA MIHADARATI!
Mapambano
makali yaliibuka hadi kupelekea Askari mmoja kujeruhiwa shingoni.
Mtuhumiwa mmoja aliwatishia Polisi kama yeye ni mwanasheria.RPC Wambura
aombwa kuchukua hatua kali kwa watuhumiwa hao.
Na Mwandishi Wetu
Jeshi
la Polisi Kanda ya Kinondoni mwishoni mwa wiki iliyopita walifanikiwa
kukamata shehena za mirungi iliyokuwa kwenye nyumba moja maeneo ya
Mwananyamala Mchangani wakiwemo watuhumiwa wawili waliotajwa kwa majina
ya Seif Ramadhani pamoja na Ahameg Mwalimu wanaonekana pichani wakiwa
kwenye kituo cha Poliai CCM Mwinyijuma.
Habari
za uhakika toka kwa mwandishi wetu aliyefika eneo la tukio dakika
chache baada ya watuhumiwa hao wawili kukamatwa na kukuta umati mkubwa
wa watu ukiwa umezunguka kituo cha Polisi huku wengi wakiwapongeza
Polisi hao waliokuwa wanaongozwa na Kamanda Makomeo ambae yupo kwenye
kikosi maalum cha kupambana na uharifu kwa kuwakama watu hao huku
wakiomba Jeshi la Polisi Kinondoni kuifanyia msako mara kwa mara nyumba
hiyo ambayo kwa hakika imekuwa kichaka cha uharifu katika eneo hilo.
Akiongea
na mwandishi wetu aliyefika eno la tuki Askari shupavu na maarufu sana
maeneo ya Kinondoni Afande Makomeo alisema kwa madai kuwa yeye si
msemaji wa Jeshi la Polisi lakini kwa maelezo zaidi mwandishi wetu afike
kwa RPC Wambura alisema" Ni kweli kama unavyoona ndugu mwandishi sisi
tupo patrol mtaani masaa 24 hivyo tulipigiwa simu na wasamalia wema na
kutuelezea kuwa kuna kundi la waharifu linashehena za mirungi ndipo
tukafika eneo hilo na kuwakamata watuhumiwa hawa wakiwa na mirungi yao"
Alisema Afande Makomeo huku umati mkubwa wa watu ukimshangilia kwa kazi
nzuri anayoifanya kamanda huyo
Hata
hivyo habari zaidi zilisema wakati wa ukamataji huo Aakari hao
walikutana na changamoto ambapo mmoja wa watuhumiwa hao alijifanyakuwa
yeye ni mwanasheria hivyo hawezi kukamatwa na mtu yeyote labda aje RPC
Wambura au Kamanda Kova na sio askari wadogo wadogo hao ambao hawana
vyeo, hali iliyompandisha hasira Afande Makomeo na vijana wake kwa
dharau hiyo licha kijana huyo mweupe kuambiwa awape kitambulisho kumbe
hakuwa na kitambulisho hali hiyo iliwafanya maafande hao kuwabeba msobe
msobe hadi kituo cha Polisi Mwinyijuma na baadae kupelekwa kituo kikuu
cha Polisi Oysterbay.
Gazeti hili lilimtafuta msemaji wa Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni RPC
Camillius Wambura.kupitia simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia tukio
hili lakini kwa bahati mbaya simu yake iliita bila kupokelewa .Credit: maskanibongotz
No comments:
Post a Comment