TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, November 25, 2015

BREAKING NEWS: DC MAKONDA KAMA RAIS MAGUFULI VILE, AWAWEKA NDANI MAAFISA ARDHI KINONDONI UNATAKA KUJUA NINI KILICHOWAPATA? MASKANIBONGOTZ LINAKUPA ISHI NZIMA..!

 Mwenyekiti wa Nyakasangwe kata ya Wazo leo hii akitangaza kwenye kiwanja cha CCM Nakalekwa juu ya Mh Paul Makonda kushindwa kufika baada ya maafisa Ardhi waliokuwa waje kuendesha zoezi la kuhakiki ardhi za wakazi hao na mafisaidi baada ya DC huyo kuamuru kuwekwa ndani kwa muda usiojulikana maafisa ardhi hao kwa kuchelewa kufika kwenye majukumu yao huku maelfu ya wananchi wakifika tangu saa kumi na mbili asubhi. visit maskaningotz

Maelfu ya wananchi wa Nakalekwa na Nakasangwe wakiwa viwanja ya CCM Nakalekwa wakimsubiri Mh Paul Makonda leo asubhi. Picha zote kwa hisaani ya mtandao wa maskanibongotz










 

























 Hivi ndivyo maelfu ya watu waliokuwa wanamsubiri Mh Paul Makonda na baadae kushindwa kutokea hali iliyowafanya wananchi hao kuwaghazabika





Na Mwandishi wa Maskanibongotz aliyekuwepo eneo la tukio.
Hata kama kusoma hujui hata picha kutizama? Hakika anaebisha acha abishe Tanzanani ilikuwa inahitaji viongozi kama akina DC Mkonda na Rais Mgufuli kiukweli kama mwendo huu utakuwa hivi basi Tanzania mpya hiyo inakuja tena miaka miwiki ijayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambae jana tu ametoka kuzungumza na maafisa wote wa Wilaya yake kuhusu kujituma kazini badala ya kusukumwa hatimae Paul Makonda leo amewatia ndani maafisa Ardhi wake wawili baada ya kuchelewa kufika kwenye majukumu yao.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi huku wakimpongeza DC huyo limetokea eneo la Nyakasangwe Serikali za mtaa ambapo leo hii kulikuwa na zoezi la uhakiki wa viwanja vya wakazi  na Nakasangwe na Nakalekwa huku maafisa Ardhi hao wakiwa wasimamizi.
MAKONDA AKASIRIKA:
Mkuu huyo wa Wilaya akiambatana na RPC Wambura wa Kinondoni, Ocd Kawe, gazri za Polisi na baadhi ya mafias usalama walifika mapema eneo hilo kama saa tano na moja kwa moja walifikia Serikali za Mtaa  wa Nyakasangwe na kupokelewa na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa huo.
Hata hivyo  wakati msafara huo wa Dc ukiwa Serikali za mtaa wa Nyakasangwe upande wa Nakalekwa tayari kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wanamshubri Mh huku wakiendelea kuungua jua kali.
Habari zaidi zilisema DC huyo akiwa bado Serikali za mtaa alisikika akimpigia simu Mkurugenzi wa Manispaa akimta angalizo kuhusu vijana wake wa kazi kwa nini wanakuwa wazembe kiasi hicho yani wananchi toka saa kumi na mbili wapo kwenye maeneo yao huku maafisa ardhi hao ambao ndiyo watu muhimu kwenye utekelezaji jukumu hilo wakiwa bado hawajafika.
Hata hivyo baada ya dakika kadhaa maafisa ardhi hao walifika wakiwa wanatetemeka  ambapo moja kwa moja Mh Paul Makonda akamuamuru OCD Kituo Cha Kawe kuwaweka ndani haraka huku akimuomba Mwenyekeiti wa Nyakasangwe kuwaomba radhi wananchi kwa dharura hiyo hadi hapo kesho saa mbili asubuhi.
Akithibitisha kutokea tuko hilo Mwenyeketi wa Nyakasangwe pichani akiwahutubia tuki maelfu ya wananchi hao na kuwaeleza kuhusu tukio hilo na kuahirisha zoezi la uhakiki viwanja hivyo kabla ya kupimiwa.
Hata hivyo katika hatua  nyingine wananchi hao wamemuomba DC Makonda kama kweli anataka kutafuta amani kwenye eneo hilo ili kumaliza mgogoro awe makini na upande wa mafisadi kwani kwa kitendo kilichoonekana leo cha kuwaleta watu wengi wasio husika ambapo ni janja ambayo watu hao wameamua kuifanya baada ya kuonba upepo mbua unawalemea wameamua kuwatengeneza watu ili waonekane hayo maeneo ni yao kukwepa kuonekana kuwa na eneo kubwa.
Wakazi wengi wa eneo hilo tayari wako kwenye vipanda vyao wakiishi na familia zao hivyo wale wote waliopo kwenye nyumba waachwe kama walivyo kwa vile tayari wameshatumia gharama nyingi kujenga maeneo hayo.
Mtandao huu wa maskanibongotz unampongeza DC huyo kwa juhudi za kutafuta amani ambapo Mungu aendelee kumuongoza ili awasaidi watanzania wenzetu hao ambao ni wanyonge wanaopigana na wenye nguvu ya pesa.

Credit:maskanibongotz






No comments:

Post a Comment