Mashabiki zaidi elfu 40 walifika jana kushuhudia uzinduzi wa radio 93.7 E-FM.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Temeke Engelbath Kiondo leo amezungumza na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake kuelezea kilichotokea jana kwenye uzinduzi wa radio hiyo mpya ya 93.7 E-FM.
Kamanda huyo alisema Jeshi la Polisi na waandaji wa tamasha hilo walipoona umati wa watu kuwa mwingi na ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kujitokeza kwa rai basi walizima mzuki mapema nusu saa kabla ya kumalizika kwa shughuri hiyo.
Hata kitendo cha kuzima muziki kabla ya muda kumalizika kiliwauzi vijana ambao walionekana ni wahuni ambao walianza kurusha mawe kwenye jukwaa pamoja na kuwashambulia Polisi kwa mawe ndipo polisi walitumia nguvu za ziada za kuwatawanya vijana hao wa kihuni kwa kuwarushia mabomu ya machozi.
Aidha katika taarifa yake Kamanda huyo alisema kuwa katika purukushani hizo polisi watatu wameumia lakini wanaendelea vizuri hadi sasa.
No comments:
Post a Comment