
Alikuwa akisafiri kutoka El Paso kwenda Dallas wakati maafisa wa uwanja wa ndege walipokuta mzigo huo ndani ya begi lake ambapo kwa mujibu wa sheria aliwekwa kizuizini na baadae kufikishwa kituo cha polisi kabla ya kuachiwa huru saa kadhaa baadae kwa mujibu wa TMZ.
Pamoja na hayo, yeye mwenyewe Wiz hakuonyesha kujali ambapo baadae alitweet picha yake akiwa chini ya ulinzi na kuonyesha hiyo ishu haijamsumbua akili kabisa.

Alipokua chini ya huo ulinzi kwa saa kadhaa Khalifa alitweet na kuonyesha picha zake akisisitiza pia kuachiwa huru.


Alipoulizwa na shabiki wake kama alipata mateso yoyote alipokua chini ya huo ulinzi, Khalifa alijibu kwamba kila kitu kilikua poa, yani alikaa vizuri tu bila matatizo.
Staa huyu aliefanya mpaka bongo imfahamu kwa sana kupitia single yake ya ‘Black and Yellow’ hii ni mara yake nyingine kukamatwa na bangi ambapo kisa kingine kilitokea November mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment