Kwenye Top 10 ya muziki mkali wa Afrika ambayo hufanyika kila Alhamisi kwenye kituo cha TV cha Ufaransa ambacho kina mamilioni ya Watazamaji Afrika (TRACE TV Urban) May 1 2014 single ya ‘number one rmx’ Diamond ft Davido imeshika nafasi ya nne.
Kwa zaidi ya wiki sita hii single imekuepo kwenye chati hizi za Trace Urban ambapo ilishika namba 1 kwa zaidi ya wiki mbili kwenye kituo hikohiko toka iachiwe rasmi January 6 2014.
Kwenye hiyo chati wiki hii number tatu imeshikwa na single ya 2Face ft T Pain, ya pili Aye ya Davido na ya kwanza ni ‘rands and nairas’ ya Emmy Gee ft Ab Crazy & Dj Dimplez.
Diamond amevunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kuingia kwenye chati hiyo na kushika nafasi ya kwanza ambapo kabla ilikua imezoeleka ni Wanigeria na Wasouth Afrika ndio wanaoongoza kwa kuishikilia.
Kwenye Exclusive interview na mtandao mmoja nchini Kenya Diamond alisema kingine alichogundua kwenye hii single ni ukubwa ilionao nchini Ghana kuliko hata Nigeria kwenyewe kwa kina Davido.
Mpaka sasa ‘number 1 rmx’ kwenye Youtube imetazamwa kwa zaidi ya mara milioni 1 na laki sita ambapo mpaka saa kumi alfajiri ya May 2 2014 ni watu 4991 walikua wameipenda kwa kulike huku 546 wakidislike.
Number 1 original ya Diamond ambayo iliwekwa kwenye mtandao September 2 2013 imetazamwa zaidi ya mara milioni mbili laki mbili na elfu 95 ambapo 5165 wamelike huku 618 wakidislike.
CREDIT: XDEEJAYZ TANZANIA
No comments:
Post a Comment